Meneja
Biashara wa CRDB Bank, Tawi la Vijana, Zaituni Manora, akitoa sera za
benki hiyo kwa wajasiriamali wa Manispaa ya Ilala, wakati wa ufunguzi wa
maonesho yao, yaliyofunguliwa na Mkuu wa Wilaya Ilala, Sophia Mjema,
Viawanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam leo. (Picha zote na
Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Baadhi
ya wafanyakazi wa CRDB Bank, wakiwa katika ufunguzi wa maonesho ya
wajasiriamali wa Manispaa ya Ilala, Viawanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar
es Salaam leo.
Baadhi
ya wafanyakazi wa CRDB Bank, wakiliandaa gari la kutolea huduma za
kibenki katika ufunguzi wa maonesho ya wajasiriamali wa Manispaa ya
Ilala, Viawanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam leo.
Ofisa
Mikopo wa CRDB Bank, Josephat Shimo akimwelekeza mmoja wa wananchi
aliyefika kwenye banda la benki hiyo katika maonesho hayo, jinsi ya
kujaza fomu za miamala ya kifedha ya benki hiyo.
Baadhi
ya wafanyakazi wa CRDB Bank, wakiwa katika picha ya pamoja ndani ya
banda lao katika maonesho hayo, wakiwa tayari kutoa huduma kwa
wajasiriamali pamoja na wananchi kwenye maonesho hayo, Viawanja vya
Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam leo.
Ofisa
Mikopo wa CRDB Bank, Josephat Shimo akiwapatia maelezo baadhi ya
wananchi waliofika kwenye banda la benki hiyo katika maonesho hayo,
jijini Dar es Salaam leo.
Ofisa
Mikopo wa CRDB Bank, Josephat Shimo (kulia), akimpatia maelezo mgeni
rasmi katika ufunguzi wa maonesho ya wajasiriamali wa Ilala, Mkuu wa
Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema (kushoto), wakati alipotembelea mabanda
mbalimbali ya huduma za kifedha pamoja na ya wajasiriamali kabla ya
kuyafungua.
Mkuu
wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema (kushoto), akimwuliza jambo Ofisa
Mikopo wa CRDB Bank, Josephat Shimo (kulia), akiwa kwenye banda la benki
hiyo, wakati akitembelea mabanda mbalimbali ya huduma za kifedha pamoja
na ya wajasiriamali kabla ya kuyafungua maonesho hayo.
Ofisa
Huduma kwa wateja wa CRDB Bank, Makao Makuu, Richard Tangazo (kushoto),
akimpatia maelezo mmoja wa wajasiriamali aliofika kwenye banda la benki
hiyo, katika maonesho hayo.
Mgeni
rasmi katika ufunguzi wa maonesho ya wajasiriamali wa Manispaa ya
Ilala, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema, akiwa meza kuu pamoja na
baadhi ya Madiwani wa Manispaa ya Ilala kabla ya kuyafungua maonesho
hayo.
Naibu
Meya wa Manispaa ya Ilala, Omar Kumbilamoto, akizungumza wakati
akimkaribisha mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema
kuzungumza katika ufunguzi wa maonesho hayo.
Mgeni
rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema, akizungumza na
wajasiriamali wa Manispaa ya Ilala, wakati akiyafungua maonesho yao,
viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Huduma za Jamii, Diwani wa Gongolamboto, Jakob Kisi,
akimkabidhi cheti cha kutambua mchango wa CRDB Bank, Meneja Biashara, Tawi la Vijana, Zaituni Manora, wakati wa ufunguzi wa maonesho hayo. CRDB Bank, ni moja ya waliodhamini na kufanikisha maonesho hayo ya wajasiriamali wa Manispaa ya Ilala.
No comments:
Post a Comment