A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Thursday, May 3, 2018

Ommy Dimpoz: Alikiba wahurumie

Msanii Omari Nyembo a.k.a. Ommy Dimpoz ambaye sasa anafanya vyema na wimbo wake 'Yanje' ambao ameshirikiana  msanii Seyi Shay kutoka nchini Nigeria, amemuomba msanii Alikiba awahurumie.

Ommy Dimpoz alisema hayo baada ya Alikiba kutangaza rasmi kuwa wimbo huo mpya wa Ommy Dimpoz ukifikisha watazamaji milioni tatu Youtube basi na yeye ataamsha dude na kuachia wimbo wake mpya baada ya 'Seduce Me' ambayo iliachiwa mwaka jana mwezi Agosti.

Baada ya ahadi hiyo ya Alikiba ndipo alipokuja Ommy Dimpoz na kumuuliza Alikiba kama atatoa ngoma zote tano kwa wakati mmoja au ataanza kuachia moja moja, hii ni ishara kwamba tayari kuna nyimbo zaidi ya tano kutoka wa Alikiba ambazo zipo tayari kwa ajili ya kuachiwa.

Aidha Msanii Alikiba akijibu moja ya swali kutoka kwa shabiki yake kupitia mtandao wa jamii ambaye alitaka kufahamu kuwa hilo dude ataliamsha lini ndipo alipojibu kuwa anawapa siku 10 tu baada ya hapo anaweza kuachia wimbo wake huo mpya.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages