Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mwita waitara
(kushoto) akivuka kivuko cha muda mfupi cha mto Mzinga jijini Dar es Salaam
jana pamoja na Viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Taifa
katika ziara ya uzindua rasmi wa operesheni ya kusajili wanachama wapya na Ukaguzi
wa Miundo mbinu iliyoharibika pamoja na kuangalia maendeleo ya ujenzi wa Daraja
la Mto Mzinga lililopo Kivule.Wapili kushoto ni Mwenyekiti wa
Chadema, Freeman Mbowe.
Diwani wa kata ya
Kivule,Wilson Molel (kushoto) akiwaeleza jambo viongozi wa Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Taifa maafa ya mvua za hivi kati
zilivyoathiri miundo mbinu ya kata ya Kivule.
Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mwita Waitara (kulia) akiwaeleza jambo viongozi wa Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Taifa jijini Dar es Salaam jana baada ya
kuwasili katika jimbo la Ukonga hilo kata ya Kivule kwa ajili ya Ukaguzi wa
miundo mbinu iliyoharibika, kutoa pole kwa wahanga wa maafa ya mvua na kuangalia
maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Mto Mzinga lililopo Kivule. Uongozi wa Chadema
Taifa ulizindua rasmi operesheni ya kusajili wanachama wapya katika Jimbo la
Ukonga na baadae mikoa mingine nchi nzima bara na visiwani.Katikati ni Katibu Mkuu Chadema,Vincent
Mashinji na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema), Freeman Mbowe
(kushoto) akizungumza na wakazi wa kata Kivule jijini Dar es Salaam jana baada
ya Kuwasili katika kata hiyo na Viongozi wa Chadema Taifa kwa ajili ya Uzinduzi
rasmi wa Operesheni ya Kusajili wanachama wapya wa jimbo la Ukonga na baadae mikoa
mingine nchi nzima bara na visiwani. Vilevile uongozi wa Chadema Taifa umefanya
Ukaguzi wa miundo mbinu iliyoharibika,kutoa pole kwa wahanga wa maafa ya mvua
na kuangalia maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Mto Mzinga lililopo Kivule.Katikati ni Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mwita Waitara.
Viongozi wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Taifa wakishuka katika mtumbwi uliotengenezwa
kienyeji unaofanya kazi ya kuvusha wakazi wa Kivule katika Mto Mzinga.
Mwenyekiti wa Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),
Freeman Mbowe (kushoto), Makamu Mwenyekiti wa Chadema Tanzania Bara, Professa Abdallah
Safari,Makamu Mwenyekiti Zanzibar, Saidi Issa Mohamed pamoja na Viongozi wengine
wa Chama wakiongoza baada ya kumaliza ziara.
No comments:
Post a Comment