A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Thursday, May 10, 2018

RAIS MAGUFULI: ASHUSHA NEEMA KITUO CHA MABASI UBUNGO SASA KAMA ULAYA














Huu ndio muonekano wa standi hiyo ya kisasa inayotarajiwa kujengwa ambayo itakuwa na sehemu za kupumzikia abiria,itakuwa na sehemu za kupaki magari madogo takribani 300,pamoja na Mabasi makubwa 200,na sehemu za biashara.

RC Makonda amemshukuru Rais Magufuli kwa kwa dhamira njema ya kusaidia kutatua kero za wananchi ambapo amewasihi wananchi wa Dar es salaam kukaa mkao wa kula kwa kuchangamkia fursa za ajira zitakazotolewa kwenye miradi hiyo. 







Stendi ya mabasi ya Abiria yaendayo mikoani Ubungo tayari  Shilingi bilioni 50  imetolewa kwa ajili ya kuanza kujengwa kituo hicho ambacho kitakuwa cha kisasa kukiwa na huduma mbalimbali za jamii ikiwemo mahoteli supermarketi pamoja na huma za kibenki.

Akizungumza leo Jijini Dar es Salaam Mkuu wa Mkoa Mhe. Paul Makonda amesema Kituo hicho kinatarajiwa kujengwa eneo la Mbezi Luis  ambapo amebainisha kuwa manispaa za jiji hilo imetengewa bajeti ya shilingi bilioni 250 kutoka mfuko wa Rais kwa ajili ya kuendeleza miradi mbalimbali.

"Tunamshukuru Rais wetu Mhe. John Pombe Magufuli kuweza kutupatia kiasi cha Shilingi Million 250,ambazo tutazitumia kuendeleza Miradi mbalimbali katika jiji letu ambapo tutaanza kwa kujenga kituo kipya cha kisasa kabisa ambacho hakijawahi kuwepo Tanzania nzima" Amesema Makonda.

Amesema walikuwa wana ndoto ya kila Halmashauri kujitengenezea vitega uchumi vitakavyoingiza kipato na kwamba ndo hiyo imetimizwa na Rais Magufuli kwani kujengwa kwa kituo hicho kutatengeneza fursa mbalimbali ikiwemo ajira na kusaidia kukuza kipato cha wananchi na Taifa kwa Ujumla.

Ameeleza kuwa Stendi ya mabasi ya Ubungo ambayo ni ya kisasa hapa nchini itakayojengwa Mbezi Luis tayari imetengewa bilioni 50 ili mkoa wa Dar es Salaam uweze kuwa na kituo bora na si tu kuwepo kwa kituo hicho bali pia stendi hiyo itaweza kutengeneza ajira pamoja na wageni mbalimbali watakaoweza kufika kwa ajili ya utalii kwani kitakuwa cha kipekee ambapo ujenzi unatarajiwa kuanza mwezi ujao.

Amesema serikali pia kwa miradi iliyokuwa ikisimamiwa na halimashauri kama vile soko la kisutu, machinjio ya Vingunguti,Soko la Mbagala Chamazi pamoja na Soko la kibada zinatarajiwa kujengwa ikiwa ni pamoja na kujengwa kwa machinjio ya kisasa kabisa ili kukuza soko la bidhaa hiyo.

"Machinjio yetu pale Vingungu tuanapaswa kujenga yawe ya kisasa ili kuboresha na kusaidia bidhaa kuuzika ndani na hata nje ya nchi kwani mahoteli makubwa wanafuata bidhaa ya nyama nje ya nchi kutokana na ubovu wa machinjio yetu"amesema Makonda.

Aidha amewataka wananchi waendelee kumpa Ushirikiano Mheshimiwa Rais kwani amedhamiria kwa dhati kuweka mazingira bora kwa wananchi wake na kukuza maendeleo ya nchi kwa kasi zaidi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages