Chama
cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Mara kimelaani madai ya askari polisi
kumuua kwa kumchoma kisu Suguta Chacha ambaye ni ndugu wa mbunge wa
Tarime vijijini (Chadema), John Heche.
Akizungumza
leo Alhamisi Mei 3. 2018 mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Samuel Kiboye
amesema haiwezekani raia anayekamatwa kwa tuhuma yoyote kufariki kwa
kipigo au sababu yoyote isiyohusika na ugonjwa wa kawaida akiwa mikononi
mwa polisi.
"Nikiwa
kiongozi na rafiki wa familia nalaani kitendo kilichofanywa na askari
aliyefanya tukio hili," amesema Kiboye alipotoa salaamu wakati wa ibada
ya mazishi ya kijana huyo inayoendelea muda huu.
Amesema
kwa nafasi yake ya uenyekiti wa mkoa, ataendelea kuwahimiza watendaji
wa Serikali, vyombo na taasisi zake kutekeleza wajibu na majukumu yao
kwa weledi wakizingatia sheria, kanuni na taratibu.
No comments:
Post a Comment