A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Thursday, May 3, 2018

Ajipeleka Polisi Baada Ya Mahindi Aliyoiba kung'ang'ania Mabegani



Mkazi wa Mbezi, Dar es salaam, Frank Japhet (23) amelazimika kujisalimisha kituo cha polisi Mlandizi, Kibaha, Pwani, baada ya mzigo wa mahindi unaokadiriwa kuwa na uzito wa kg 20, anaodaiwa kuuiba kung'ang'ania kichwani.

Kwa maelezo ya mtuhumuwa huyo aliyoyatoa kituoni hapo, mzigo huo wa mahindi, uliofungwa kwenye kiroba aliuiba kwa mama mmoja eneo la mtaa wa Nyambwiro, Mlandizi, Kibaha, Pwani majira ya saa 7.00 usiku wa kuamkia leo.

Amesema, alipoondoka na mzigo huo hadi eneo la stendi ya Mlandizi alipokuwa auache kwa mwenzake ili arudie mzigo mwingine, mzigo huo uling'ang'ania kichwani.

Amesema, alijitahidi kufanya kila aliloweza ili mzigo huo utoke kichwani ikiwa ni pamoja na kulala ili akinyanyuka ubaki chini lakini aliponyanyuka, alinyanyuka nao kichwani!

Baada ya kuzunguka nao kwa muda mrefu, alidai alichoka akalazimika kujisalimisha polisi ili asije akauawa na raia wenye hasira watakapobaini kuwa ni mwizi.

Mpaka sasa yuko kituo cha polisi Mlandizi na mzigo wake kichwani akisubiri mwenye mali aliyoiiba ambaye jeshi la polisi Mlandizi tayari limemuita afike kituoni hapo.

Tutawaletea taarifa zaidi za tukio hilo.

Na Masau Bwire-Mzalendo.

03/05/2018

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages