Mkuu
wa Wilaya ya Kigamboni Mh.Hashim Mgandilwa ameondoa hali ya taharuki
iliyokuwa imetanda miongoni mwa wananchi wa Kata ya Kibada waliowekewa
alama ya kubomoa majengo yao na wakala wa barabara (TANROADS) mbali na kununua viwanja hivyo kihalali kutoka wizara ya ardhi.
Akizungumza
na wananchi hao kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jana kwenye ofisi
za Kata ya Kibada Mh.Mgandilwa amesema kuwa ofisi yake na wataalamu
hawapo tayari kuona wananchi wao wanaonewa.
Aliongeza
kuwa mgongano huo umebainika kwenye mradi wa ujenzi wa barabara uliopo
kwenye hatua za awali na ubainishaji wa mipaka wa Tanroads unaolenga
kujenga barabara kiwango cha lami kuanzia Kibada-Somangila hadi Kimbiji.
Mgandilwa
alisema kuwa wizara ya ardhi ilikuwa na mradi wa viwanja ishirini elfu
vilivyouzwa kwa wananchi kihalali ambapo baada ya Tanroads kubainisha
mipaka yake ndipo ilipobainika kuwa wizara ya ardhi iliuza viwanja vyake
hadi kwenye hifadhi ya barabara.
"Viwanja
hivi vilinunuliwa wizara ya ardhi ambapo wananchi walikuwa na uhakika
wa usalama wa viwanja vyao kutokana na kununua kwene wizara husika, leo
hii kuja kuwawekea alama ya kubomoa sio haki, mwananchi anakuwa
anawajibishwa kwa kosa ambalo si lake ndiomaana tumekutana hapa ili
tuweze kuona namna gani tunaweza kufikia muafaka" Alisema Mkuu wa
Wilaya.
Aliongeza kuwa wao kama Serikali wameona ni bora kuzungumza na wananchi kwasababu Serikali haipaswi kukinzana na sheria badala yake inaangalia mahali ambapo pamekosewa na kurekebisha.
Aidha
Mkuu wa Wilaya aliwataka wananchi wote waliowekea alama za kubomoa
majengo yao ndani ya siku 90 kufika ofisini kwake siku ya jumamosi
tarehe 5/5/2018 ambapo kutakuwa na wataalamu kutoka wizara ya Ardhi na
Tanroads ili kuona namna bora ya kufikia muafaka.
Wakati
huohuo Mkuu wa Wilaya amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye
hamasa na kuthaminiwa hususani wananchi ambao watapitiwa na ujenzi wa
mradi wa kituo cha kupoozea umeme ambapo italazimika kusimika nguzo za
umeme ambazo hazitaruhusu uwepo wa makazi ya aina yeyote.
Mkuu
wa Wilaya alisema kuwa, ni vyema wakajitokeza ili kuondoa malalamiko na
adha zinazazoweza kuzuilika kwenye hatua za utambuzi na uthamini ili
kulipwa fidia kwasababu nishati ya umeme inahitajika kwa kiwango kikubwa
kutokana na Wilaya ya Kigamboni kukosa umeme wa uhakika, na kuwa
waathirika wa kwanza pindi inapotokea hitilafu kidogo kwenye vituo
vinavyotegemewa kwa sasa.
"Nawaomba
ndugu zangu mjitokeze pindi mtakapohitajika kwenye zoezi la utambuzi na
uthamini, Wilaya ya kigamboni tunahitaji umeme wa uhakika ili tuweze
kuwa na viwanda na uwekezaji wenye tija kutokana na kuwepo kwa umeme wa
uhakika" Alisema Mh.Mgandilwa
Mradi wa kituo kidogo cha kuupozea umeme kinajengwa Dege kata ya Somangila ambapo hadi kufikia mwaka 2020 unatarajiwa kuwa umeanza kazi huku Kata
tatu za Kibada,KisaraweII na Somangila kwenye mitaa 6 inatarajiwa
kupitiwa na nguzo hizo zenye umeme mkubwa ambao hauruhusu kuwepo kwa
makazi yeyote kwa usalama wa wananchi wa maeneo hayo.
Imeandaliwa na:
Kitengo cha Teknolojia, Habari na Mawasiliano
Halmshauri ya Manispaa ya Kigamboni
03/05/2018
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mh.Hashim Mgandilwa mwenye
kofiaakizungumza na wakazi wa Kibada kwenye mkutano wa hadhara
uliofanyika jana.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mh.Hashim Mgandilwa akisistiza kuwa Sheria itafuatwa kuhakikisha wananchi wanapata haki yao.
Mkuu wa wilaya ya Kigamboni Mh.Hashim Mgandilwa na wananchi wa kibada wakisoma ra,mani ili kubaini mipaka .
Diwani
wa Kata ya Kibada Mh.Amin Sambo akishiriki kuchimba eneo linalodaiwa
kuwa na jiwe la mpaka kwenye eneo la mkazi wa Kibada wakati walipokuwa
wakitafuta mawe ya Mipaka.
Kamati
ya ulinzi na usalama na waanchi wakizulu kwenye moja ya nyumba
iliyowekwa alama ya kubomoa na wakala wa barabara Tanroads ili kubaini
mpaka uliopo.
Mthamini wa Manispaa ya Kigamboni Bw.Mpoki Daimon akifafanua taratibu
za uthamini na ulipwaji fidia kwa wananchi wa Kata ya Somangila Mtaa wa
Dege.
Baadhi ya wananchi na wataalamu mbalimbali walishirki kwenye mkutano huo wa hadhara Kibada.
No comments:
Post a Comment