A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Tuesday, May 29, 2018

Belle 9 aelezea Ishu ya kukimbia mji


Msanii wa muziki wa Bongofleva Belle 9, amesema kuwa amehamia nje ya mji baada ya kufunga ndoa na hajahama Jijini kama ambavyo taarifa zilivyoenea.

Belle 9 amefunguka kupitia eNewz ya EATV kuwa alihama baada ya kufunga ndoa hali iliyosababisha pia kupunguza mitoko ya mara kwa mara lakini yupo Dar es salaam.

“Nilikuwa naishi Kijitonyama nimehamia nje ya mji na labda kwakuwa sitokei sana kwenye matukio mengi ndiyo maana wanahisi nimehama mji lakini nipo hapahapa”, amesema Belle9.

Belle 9 pia ameongeza kuwa anafurahia maisha yake ya ndoa na hakuna ukweli kuwa ukioa lazima umuimbie mkeo kama watu wanavyodai. Msikilize hapo chini Belle9 amefunguka zaidi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages