A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Monday, April 30, 2018

Serengeti Boys wanyakua ubingwa wa CECAFA U- 17


Timu ya taifa ya Tanzania ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) imeibuka na ubingwa wa CECAFA U-17 baada ya kuifunga timu ya vijana ya Somalia mabao 2-0 katika fainali iliyopigwa huko Burundi.


Serengeti Boys imecheza vizuri mchezo huo wa fainali na kufanikiwa kuongoza kwa bao moja hadi mapumziko kabla ya kuongeza bao la pili kipindi cha pili na kujihakikishia ubingwa huo.

Mabingwa hao wapya wa Afrika Mashariki na Kati, wamekabidhiwa kombe hilo na mgeni rasmi wa fainali hiyo ambaye ni Rais wa shirikisho la soka barani Africa Ahmed Ahmed.

Vijana hao wametinga fainali hiyo baada ya kuwatoa timu ya Taifa ya Kenya U17 kwa jumla ya mabao 2-1 katika mchezo wa nusu fainali uliopigwa Alhamisi. Wakati Somalia imeingia fainali kwa kuifunga Uganda 1-0.

Moja ya timu zilizofungwa na vijana hao katika hatua ya makundi ni pamoja na Sudan na Uganda. Katika michuano hii timu ya taifa ya vijana ya Zanzibar (Karume Boys) iliondolewa kutoka na kuwa na wachezaji wenye umri mkubwa.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages