Mganga Mkuu wa Serikali-Wazara ya Afya, Prof. Mohammad Bakari Kambi,
akiongea katika uzinduzi wa miradi mikubwa miwili (PAVIA na PROFORMA),
inayolenga kuweka mifumo ya kuthibiti ubora na viwango vya madawa yanasambazwa
na kutumiwa katika masoko ya Tanzania na nchi zingine za Afrika. (Picha na
Mpiga Picha Wetu).
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA).
Adam Fimbo, akiongea katika uzinduzi wa miradi mikubwa miwili (PAVIA na
PROFORMA), inayolenga kuweka mifumo ya kuthibiti ubora na viwango vya madawa
yanayosambazwa na kutumiwa katika masoko ya Tanzania na nchi zingine barani
Afrika.
Mamlaka ya chakula na dawa nchini (TFDA) kwa kushirikiana na
taasisi mbalimbali Afrika jana wamebuni miradi miwili mikubwa yenye lengo ya
boresha, kuhakiki na kufuatilia ubora na viwango vya madawa yanayosambazwa na
kutumiwa na binadamu.
“Lengo kuu ni kumlinda mlaji na watumiaji wa dawa,” amesema
Mganga Mkuu wa Serikali Kutoka Wizara ya Afya, Profesa Muhammad Bakari Kambi,
wakati wa ufunguzi wa miradi ya PAVIA na PROFORMA, yenye lengo la kuweka mifumo
ya kuthibiti ubora wa madawa barani Afrika. Miradi hii inafadhaliwa na Programu
ya Maendeleo ya Majaribio ya Dawa Kwa Nchi za Ulaya na Afrika (EDCTP).
Akifafanua, Mganga Mkuu wa serikali amesema miradi hii itasaidia
pia kufuatilia kwa urahisi madhara ya madawa yanayosambazwa na kutimiwa katika
masoko.
‘’Miradi hasa itaweza kufanya ufuatiliaji matukio baada ya
mgonjwa kutumia dawa husika na kuona ni kwa namna ipi imeweza kumsaidia au
imemletea madhara baada ya kutumia ila hatua za haraka ziweze kuchukuliwa,’’ alisema
Profesa Kambi.
Alisema kwamba miradi hii kwa pamoja itaweza kushughulikia
usalama wa dawa kwa watumiaji na kufanya kwa kina udhibiti wa dawa bandia
katika sehemu zote za nchini pamoja na maeneo ya mipakani.
Katika utekelezaji wa miradi hii kwa pamoja itatoa fursa kwa
watumishi wa umma kujifunza jinsi miradi inavyoweza kufanya kazi na upatikanaji
na utoaji wa taarifa muhimu tena kwa wakati katika kupambana na dawa bandia
nchini.
Profesa Kambi aliongeza kwamba miradi inatarajiwa pia kuanza
kubuni mitaala maalum itakayotumiwa na vyuo vikuu nchini katika juhudi za
kuanza kuwandaa wanafunzi mapema jinsi ya kukabiliana na matokeo ya dawa kwa
mgonjwa.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Dawa, kutoka Mamlaka ya chakula
na dawa nchini, Adam Fimbo amesema usalama wa dawa nchini upo na mamlaka
kupitia miradi hiyo miwili wataweza kuendelea kuboresha huduma za upatikanaji
na udhibiti wa dawa hafifu na bandia katika soko la dawa nchini.
.
‘’Tumeungana na nchini kadhaa katika uanzishwaji na utekelezaji
wa miradi hii katika harakati za kuweza kupambana matokeo baada ya mgonjwa
kutumia dawa na kuweza kutengeneza mifumo inayoweza kuleta taarifa mapema na
kuweza kuwasiliana kwa haraka na kubadilishana uzoefu,’’ aliongeza Fimbo.
“Sisi kama mamlaka ya chakula na dawa jukumu letu ni kusajili
dawa, kuhakiki na kusiruhusu zitumike nchini lakini pia kuhakikisha
tunafuatilia kwa karibu matokeo ya dawa kwa wagonjwa na tukigundua hazitowi
matokeo chanya tunaziondoa mara moja,’’ alifafanua
Alifafanua kwamba miradi hiyo miwili inatasaidia kwa uhakika
kutengeneza mifumo ya ufuatiliaji wa dawa kwenye soko na kuwajengea uwezo
taasisi mbalimbali za afya nchini na kupelekea miradi hii kwenye mitaala ya
vyuo vikuu.
Kwa upande wake, Afisa Mradi wa EDCTP, Bibi. Michelle Nderu
alisema kwamba wameamua kufadhili miradi hiyo ili kuleta uzoefu kutoka kwenye
nchini zilizoendelea ili kuboresha matumizi sahihi ya dawa kwa binadamu.
‘’Miradi hii itaweze kuongeza nguvu zaidi katika maeneo mengi
katika nchini kadhaa chini ya jangwa la Sahara katika juhudi za kumlinda
mgonjwa dhidi ya dawa bandia,’’ alisema.
Nderu aliongeza kwamba lengo la miradi hii ni kusaidia
kuimarisha mifumo ya kitaifa ya afya kwa nchini za Afrika ili kuzalisha dawa
mpya na zenye usalama na ubora wa uhakika na pia ufuatiliaji katika masoko.
Miradi ya PAVIA na Profoma inatekelezwa na kadhaa, ikiwa ni
pamoja na Kenya, Italy, Uholanzi, Rwanda, Swedena na Ethiopia.
No comments:
Post a Comment