Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Vingunguti, Omary Kumbilamoto amewashukuru Viongozi wa Manispaa ya Ilala na wananchi wa Wilaya hiyo kwa ushirikiano wao walio onesha katika kisomo cha hitima ya Mama yake mzazi iliyofanyika Kijijini Kauzeni Wilayani Kisarawe.
Kumbilamoto Ameyasema hayo leo Kijijini Kauzeni wakati wa Hitima ya Marehemu Mama yake na kuwataka kuendelea na moyo huo wa kusaidia na kufarijiana katika wakati wa matatizo bila kujali itikadi zao.
"Napenda pia ni mshukuru Shekh mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Shekh Mussa Alhadi na pia nimtakie afya njema nimeambiwa anaumwa na ametuma Mwakilishi wake , pia natoa shukrani zangu kwa mkuu wa wilaya ya Ilala Mhe.Sophia Mjema na uongozi wa Halimashauri ya Manispaa ya Ilala kwa ushirikiano wao Inshaallah Mwenyezi Mungu awazidishie "Amesema
Nao baadhi ya viongozi wa Dini na wananchi waliohudhuria hitima hiyo wamemzungumzia Kumbilamoto la moto kuwa ni kiongozi wa tofauti anayejishusha bila kujali cheo na madaraka aliyo nayo na kuwa ni mfano wa kuigwa katika Jamii.
" Ni agharabu Sana kwa viongozi kuwa na moyo kama wa huyu Naibu Meya kwakweli mi na muombea mwenyezi Mungu ili aweze kuambukiza na wengine wawe na moyo kama yeye na washirikiane." Amesema mwananchi ambaye ameomba jina lake lihifadhiwe.
No comments:
Post a Comment