Naibu Meya wa Ilala ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Vingunguti Omary Kumbilamoto amepokea msaada wa vyakula kutoka Jumuiya ya Lions na food Bank kwa ajili ya wahanga wa mafuriko katika kata hiyo.
"Leo nimepokea vyakula kwa ajili ya waathirika wa mafuriko kutoa ni moyo sio utajiri niwashukuru jumuiya ya Lions na food Bank kwa kuja kutuletea misaada hii kwa ajili ya wananchi wetu" Amesema Kumbilamoto.
Aidha amemshukuru Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda kwa kuwatembelea wahanga hao wamafuriko ambapo jumla ya familia 120,hazina makazi kutokana na mvua zilizonyesha usiku wa kuamukia Jumapili April 18, mwaka huu na kupelekea nyumba zao kubomoka.
" Nimshukuru Mkuu wa mkoa Mhe.Makonda kwa kuja kuwatembelea waathirika hawa na kuwaelekeza wadau waje kutusaidia asiye shukuru kwa kidogo hata akipewa kikubwa hawezi kushukuru"Amesema.
Vilevile Kumbilamoto ameishukuru Jumuiya hiyo kujitoa kwa ajili ya kuwasaidia wahanga hao wa mafuriko na kuwataka wadau wengine kuendelea kujitokeza kwani kutoa ni moyo na si Utajiri.
Tazama picha Mbalimbali za vyakula hivyo.
No comments:
Post a Comment