RC Makonda akizungumza jambo na Ahamed Albaity
Rc Makonda akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla hiyo
Rc Makonda akimkabidhi tiketi nne,mmoja wa ndugu anayesafiri na Ahamed
Machozi ya furaha leo yameitoka familia ya kijana Ahmed Albaity
baada ya kukamilika kwa Safari ya matibabu kwa kijana wao kuelekea Nchini China
safari iliyofanikishwa kwa jitiada binafsi za Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe.
Paul Makonda ambae amejitolea kugharamia fedha ya Usafiri, Matibabu na Malazi
kwa kijana huyo na hatimae jioni ya leo RC Makonda amemsindikiza Ahmed Uwanja
wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere tayari kwa safari.
Ahmed alipangiwa na Madaktari kwenda kupatiwa Matibabu China
tokea Miaka miwili iliyopita lakini hakuweza kwenda kutokana na kushindwa
kumudu gharama lakini kupitia jitiada binafsi za RC Makonda amefanikisha Safari
ya Matibabu kwa Ahmed.
Ahmed Albaity amesafiri jioni ya leo akiongozana na wasaidizi Watatu
ambapo RC Makonda amewafanikishia kupata fedha ya Tickets Nne za Ndege (first
class), fedha ya matibabu na fedha ya kujikimu ambapo kwa ujumla ni zaidi ya Million
107.
RC Makonda amesema ataendelea kumsaidia Ahmed kwa kadiri ya
uwezo wake ili aweze kurudi katika Hali yake ya kawaida ambapo amewashukuru
wadau wote waliomchangia hadi kufanikisha safari hiyo.
"Nafasi ya Ukuu wa Mkoa sio yangu bali ni ya watu na watu
wana changamoto zao hivyo tunalazimika kutoka kwenda kuona mahitaji ya wananchi
na hatimae waone thamani ya uongozi na Serikali yao, hatuna bajeti lakini Mimi
kama Makonda niliniliona vyema niwatafute Marafiki zangu ili tumsaidie ndugu
yetu Ahmed apate matibabu na kurejesha tabasamu, ninayo furaha kusema
tumefanikiwa kupata Dola 52,000 sawa na zaidi ya Million 107" Alisema RC
Makonda.
RC Makonda amewasihi wananchi kuwa na Moyo wa kusaidiana kwenye
matatizo na kuombeana heri.
Kwa upande wake Ahmed amemshukuru Rais Dr. John Magufuli kwa
kumteua RC Makonda kuongoza Mkoa wa Dar es salaam ambapo kupitia yeye amefanikisha
ndoto yake ya kupatiwa matibabu Nje ya Nchi.
Aidha amesema wana Dar es salaam wanapaswa kujivunia kupata
bahati ya kipekee ya kuwa na kiongozi imara anaejali wananchi wake pasipokujali
Dini wala kabila.
No comments:
Post a Comment