Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amefunguka na kusema watu
wanaojifanya kutaka kuandamana wataweza kufanya hivyo kipindi ambacho
yeye hatakuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam au hakiwa ameondoka ila
vinginevyo hawawezi kuthubutu kuandamana.
Makonda
amesema hayo akiwa anahotubia kwenye moja ya mkutano uliofanyika Dar es
Salaam na kusema kuwa watu wengine ambao wanapiga sana kelele kuhusu
maandamano hayo na kutaka kuvuruga amani ya nchi ndiyo wanapata fedha
nyingi kutoka wa wafadhili wao ambao hawataki Mkoa wa Dar es Salaam
ubaki salama.
"Kuna
kakundi hapa kanahangaika kweli usiku na mchana wengine wanahangaika
kutumia mitandao ya kijamii kutukana viongozi, kuhamasisha sijui wanaita
nini sijui maandamano nawapa pole sana, watafanya labda mimi nikiondoka
nikiwa siyo Mkuu wa Mkoa .....kwenye huu Mkoa hiyo mipango mipango yao
watafanya labda mimi nikiwa sipo lakini amani ya mkoa wa Dar es Salaam
ni muhimu sana" alisemana kuongeza;
"Amani
ni muhimu sana kuliko propaganda za kisiasa na niwaambieni tu wengine
wakipiga kelele na kutokea kwenye 'front page' kwenye magazeti ndiyo
wanapata mshahara zaidi, wanapata donor kutoka kwenye baadhi ya mataifa
yasiyotakia amani taifa letu kwa hiyo lazima tujue tunaye adui
tunayeishi naye kama Mtanzania lakini amebeba majukumu ya mataifa
yasiyoitakia amani taifa letu" alisisitiza Makonda
No comments:
Post a Comment