Rc Makonda akimjulia hali kijana Ahmed alipomtembelea kumjulia hali pia kumpa tiketi ya ndege kwaajili ya kwenda China kwa matibabu
Rc Makonda akimkabidhi Viza ndugu ya Ahmed kwaajili ya kuanza safari ya kwenda china kwaajili yakupata matibabu
Ndoto na shauku ya kijana Ahmed Albaity alieteseka kwa zaidi ya Miaka
10 Kitandani kwa kushindwa kumudu gharama za matibabu leo imebadilika kuwa
furaha baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda kumkabidhi
Tiketi za Ndege za watu Wanne kwaajili ya safari ya kwenda kupatiwa matibabu
Nchini China kwenye Hospital ya Beijing Puhua International huku akijitolea pia
kugharamia fedha za Matibabu na Malazi.
RC Makonda alitoa ahadi kumsaidia Ahmed Albaity wakati wa Zoezi
la Upimaji Afya Bure kwenye Meli ya Jeshi la China mwishoni mwa Mwaka Jana
baada ya kugundulika Ahmed anahitaji Matibabu Maalum ambayo hayapatikani kokote
kule duniani isipokuwa China, jambo lililomfanya RC Makonda kutokwa na Machozi
na Kuhaidi Kumpeleka kwenye matibabu kwa gharama yoyote ile Maumivu na Mateso
anayopitia kijana huyo.
Ahmed Albaity anasumbuliwa na tatizo la uti wa mgongo baada ya
kuanguka na kuvunjika Shingo alipokuwa akiogelea ambapo kwa sindano moja pekee
inagharimu Dollars 26,000/= sawa na shillingi million 52.
RC Makonda amesema Ahmed atasafiri Nchini China Siku ya Jumapili
akiongozana na watu watatu wa kumsaidia kumuhudumia ambapo gharama zake ni
zaidi ya Shilingi Million 100.
Aidha RC Makonda amesema Shauku yake ni kugusa maisha ya
Mwananchi hata kama ni mmoja atakaekwenda mbele za Mungu na kusema Asante Mungu
kwa kutupatia viongozi wetu, ifike mahali tumtumikie Mungu katika nafasi zetu,
na katika hilo watu wote watakuwa Sawa na tutawahudumia bila kutarajia chochote
kutoka kwao kama sehemu ya utumishi wetu ambapo amewashukuru watu wote waliomchangia
na kufanikisha matibabu.
Hata hivyo RC Makonda ametoa wito kwa wananchi wa dini zote kumuombea
Ahmed ili aweze kupona na kuendelea na shughuli za ujenzi wa Taifa.
Kwa upande wa Ahmed Albaity amemshukuru RC Makonda kwa moyo wa
ukarimu aliouonyesha ambapo ameeleza kuwa ameishi kwa mateso muda mrefu
kutokana na kukosa uwezo wa kumudu gharama za matibabu.
Aidha amesema alipokuwa akiomba watu wamchangie wapo waliokuwa
wakimvunja moyo kwa kumwambia hawezi kupona lakini RC Makonda ameonyesha moyo
wa kipekee.
Rc Makonda akitoa maelekezo kwa ndugu ambao wataambatana na Ahmed katika safari hiyo.
No comments:
Post a Comment