Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe
Magufuli akikata utepe kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa
mradi wa Reli ya Kisasa itakayotumia umeme Standard Gauge (SGR)
itakayotoka mkoani Morogoro hadi Makutupora Dodoma katika eneo la
Stesheni ya Ihumwa nje kidogo ya mji wa Dodoma. Wengine katika picha ni
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Profesa Makame Mbarawa pamoja na Balozi wa Uingereza hapa nchini Sarah
Cooke wakishuhudia.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akifunua kitambaa wakati akiweka jiwe la msingi ujenzi wa mradi wa Reli
ya Kisasa itakayotumia umeme Standard Gauge (SGR) itakayotoka mkoani
Morogoro hadi Makutupora Dodoma katika eneo la Stesheni ya Ihumwa nje
kidogo ya mji wa Dodoma.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akifunga kifuniko mara baada ya kutumbukiza karatasi ya majina ya
viongozi mbalimbali waliofanikisha ujenzi huo kama kumbukumbu katika
uwekaji wa jiwe la msingi la Reli ya Kisasa(SGR) itakayotoka mkoani
Morogoro-hadi Makutupora Dodoma.
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa akiweka saruji iliyochanganywa na kokoto kwenye
jiwe hilo la msingi la ujenzi wa Reli ya Kisasa mkoani Morogoro-hadi
Makutupora Dodoma yenye urefu wa km 422 katika eneo la Ihumwa stesheni
mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe
Magufuli akiweka saruji iliyochanganywa na kokoto kwenye jiwe hilo la
msingi la ujenzi wa Reli ya Kisasa kutoka mkoani Morogoro-hadi
Makutupora Dodoma yenye urefu wa km 422 katika eneo la Ihumwa stesheni
mkoani Dodoma.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akikata utepe pamoja Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuashiria uzinduzi wa
ujenzi wa Reli ya Kisasa ya umeme kutoka mkoani Morogoro-hadi Makutupora
Dodoma yenye urefu wa km 422 katika eneo la Ihumwa stesheni mkoani
Dodoma. Wengine katika picha ni Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson, Waziri wa
Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Pro. Makame Mbarawa, Mkurugenzi
mtendaji wa Shirika la Reli TRC Masanja Kadogosa pamoja na viongozi
wengine.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akikagua mfano wa Reli hiyo ya Kisasa itakayotumia umeme mara baada ya
kuweka jiwe la msingi katika eneo la Ihumwa stesheni mkoani Dodoma.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akiwasalimia baadhi ya wabunge waliofika kwenye uzinduzi wa Reli hiyo ya
Kisasa SGR itakayo toka Morogoro hadi Dodoma.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akiwasalimia wananchi mara baada ya kuweka jiwe la msingi la Reli hio ya
Kisasa katika eneo la Ihumwa Stesheni mkoani Dodoma.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akiwashukuru madereva wa magari yatakayofanya kazi ya ujenzi wa reli
hiyo ya kisasa SGR itakayo toka Morogoro hadi Dodoma.
Sehemu ya wananchi mbalimbali waliohudhuria sherehe hizo za uwekaji wa jiwe la msingi.
Treni ya zamani ikipita katika Reli za zamani katika eneo la Ihumwa stesheni mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe
Magufuli akiwasalimia wananchi wakati akiwasili katika eneo la Ihumwa
Stesheni kwa ajili ya uwekaji wa jiwe la msingi.
Mtendaji
Mkuu wa Shirika la Reli TRC Masanja Kadogosa akitoa maelezo ya mradi
huo wa Reli ya kisasa ya umeme kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli PICHA NA IKULU
No comments:
Post a Comment