Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kisare Makori, akifungua pazia kuashiria uzinduzi rasmi wa ujenzi wa mradi wa kuchakata majitaka unaojengwa katika Kata ya Mburahati, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, leo jijini hapa.
Mhandisi wa mradi wa uchakataji maji taka Mburahati, MOdekai Sanga, akifafanua jambo juu ya mradi huo kwa mgeni rasmi.
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kisare Makori, (kushoto) akisalimiana na Diwani Kata ya Mburahati, Yusuph Yenga, wakati wa uzinduzi rasmi wa ujenzi wa mradi wa kuchakata majitaka unaojengwa katika Kata ya Mburahati.
Afisa Uhusiano wa Shirika la Majisafi na Majitaka (DAWASA na Dawasco), Neli Msuye, (katikati) akiteta jambo na Mratibu wa Mradi, Laura Bright Davies (kushoto) wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa ujenzi wa mradi wa kuchakata majitaka unaojengwa katika Kata ya Mburahati.
Mratibu wa Mradi, Laura Bright Davies, akiwasalimia wananchi wa kata ya Mburahati katika hafla hiyo
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kisare Makori, akipanda Mti.
SERIKALI
Mkoani Dar es Salaam, imesema inamatumaini makubwa ya kuwapatia wakazi wake huduma ya maji kwa asilimia 95
ifikapo mwaka 2010 na asilimia 100 ifikapo mwaka 2025.
Pia, imesema kwa kushirikiana na Mamlaka zake za Majisafi na Majitaka (DAWASA
na Dawasco) imejizatiti kikamilifu
kukabiliana na changamoto ya uondoaji wa majitaka ambapo kwa sasa ni
asilimia 10 tu ya wananchi mkoani humo wanapata huduma hiyo.
Akizindua
ujenzi wa mradi wa kuchakata majitaka
unaojengwa katika Kata ya Mburahati, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Paul Makonda, Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kisare Makori, alisema sera ya serikali ni kuwafikishia huduma ya maji wananchi wake
wote mkoani humo.
Makori
ambaye pia alikuwa akihutubia katika
kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Maji, mkoani humo, alisema, matumaini hayo
yanatokana na miradi mikubwa
iliyokamilika na mipango inayoendelea
kutekelezwa na serikali kupitia
DAWASA na DAWASCO na Ofidi ya Mkuu wa Mkoa.
“Kukamilika
kwa mradi mkubwa wa Ruvu Chini
ambao umeongeza upatikanaji
wa maji kutoka lita milioni 182 kwa siku
na kufikia lita milioni 270.
Kukamilika
kwa mradi huu kutaongeza upatikanaji wa
maji katika maeneo ya Bagamoyo,Tegeta,
Mbweni, Kinondoni, Chuo Kikuu, Kunduchi, Kawe, Mikocheni na maeneo ya katikati
ya jiji,”alisema Makori.
Pia,
kukamilika kwa mradi mkubwa wa Ruvu Juu ambao alisema umeongeza upatikanaji wa maji kutoka lita milioni 82
kwa siku na kufikia lita milionui 196 kwa siku.
“Kumeongeza
upatikanaji wa maji katika maeneo ya Kibaha, Kibamba, Mbezi, Kimara, Ubungo na
Tabata,”alifafanua.
Makori
alisema kukamilika kwa visima 20 vya Kimbiji na Mpera vitaongeza
upatikanaji wa huduma ya maji kwa lita milioni 250 kwa siku
maeneo yatakayohudumiwa na Wilaya ya Kigamboni, Temeke na baadhi ya maeneo ya
wilaya ya Ilala.
“Kukamilika
kwa miradi ya visima10 vya mpango wa maendeo ya sekta ya maji ambapo visima tisa vilivyojengwa na manispaa vinahudumia watu zaidi ya 300,000,”alisema.
Alisema hadi
sasa kumekuwa na ongezeko kubwa la
wateja waliounganishiwa huduma ya maji kutoka 123,00 mpaka 268,000.
Kuhusu suala la mfumo wa majitaka, Makori, alisema,
kukamilika kwa ujenzi wa miradi midogo
ya kusafisha majitaka katika kata ya
Toangoma na Mburahati itasaidia kwa
kiasi kikubwa katika uondoaji wa majitaka katika makazi ya watu .
“Kwa sasa ni
asilimia 10 tu ya wakazi ndiyo wanapata
huduma ya kuondolewa majitaka lakini
serikali kwa kuishirkiana na
DAWASA na Dawasco, pamoja na wadau ipo
katika hatua za utekelezaji miradi mikubwa,”alisema Makori.
Alitaja
mradi wa mfumo wa uondoaji majitaka kwa
wakazi wa mkoa wa Dar es Salaam, ambao utajengwa katika eneo la Jwangani utakaokuwa na uwezo wa kusafisha lita za
ujazo 200,000 kwa siku.
“Mradi wa
Kurasini utakuwa unasafisha lita 11,000 kwa siku, Mbezi Beach utasafisha lita
za ujazo 16,000,”alisema.
Aliongeza;
‘Mradi huu utahusu upanuzi wa mfumo wa
majitaka maeneo ya katikati ya jiji,
ujenzi wa mfumo mpya Ilala , Ubungo na
Kinondoni,”
Alisema
mradi wa maji na usafi wa mazingira unaofadhiliwa kupitia program ya Maendeleo ya Sekta ya Maji
(WSDP II) utahusu ujenzi wa mifumo 50 ya
kukusanya na kusafisha majitaka na
ujenzi wa vyoo vya kisasa na utatekelezwa katika kipindi cha miaka mitano.
Mhandisi wa
mradi wa uchakataji maji taka Mburahati,
MOdekai Sanga alisema utakuwa na uwezo wa kuhudumia wananchi
40,000 na utagharimu sh.milioni 95.
Burudani zikiendelea
Wanahabari wakiwajibika katika hafla hiyo.
No comments:
Post a Comment