A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Saturday, March 10, 2018

Hospitali ya Aga Khan yazidi kung'ara yazindua kituo kipya kimara



Karibu tawala Wilaya ya Ubungo  James Mkumbo, akikata utepe kwa ishara ya kuzindua kituo kipya cha hospitali ya Aga Khan Kimara.

Mkurugenzi mkuu wa magonjwa ya moyo,ambaye pia ni Daktari bigwa Mustapha kapumi,akizungumza na kutoa historia ya Hospitali hiyo na kuwataka wakazi wa Kimara kufika kutibiwa katika hospitali hiyo kwani itatoa huduma kwa bei nafuu na rafiki kwa kila mmoja.
Mkurugenzi wa Uuguzi,Taasisi ya Huduma ya Afya Aga Khan Tanzania Dkt. Lucy Hwai akizungumza, na kufungua tukio la uzinduzi wa kituo kipya cha hospitali hiyo na kutoa shukrani na pongezi za kusogeza huduma ya Afya karibu na wananchi.



Dr. Omar Sherman(Head of Pathology AKHST) akizungumza na kuwataka wakazi wa Kimara kufika kupata huduma katika kituo hicho kilichozinduliwa leo na kitatoa huduma rafiki na nzuri kwa kila mwananchi




Baadhi ya wafanyakazi wa hospitali hiyo,pamoja na wageni waalikwa waliohudhuria katika tukio la uzinduzi wa hospitali ya Aga Khan Kimara Jijini Dar es Salaam.

Na Anna Chiganga Utouh news.


Hospitali ya AGHAKAN  yazindua kituo kipya kimara wilaya ya Ubungo jijini dar es salaam,na kuombwa kuanzisha huduma ya upasuaji hasa upasuaji wa uzazi ili kuwawezesha wakina mama kupata huduma karibu kwa lengo la kuokoa maisha ya mama na mtoto.

Akizungumza kwa niaba ya mgeni rasmi Katibu tawala Halmashauri ya manispaa ya Wilaya ya Ubungo James Mkumbo amesema wanashukuru sana uongozi wa hospitali hiyo kuweza kuwaletea huduma ya Afya karibu katika manispaa hiyo ambapo itarahisisha huduma za afya kwa wakazi wa wilaya hiyo na kuomba kujengwa kwa jengo la uzazi ili kurahisisha huduma ya kina mama kujifungulia katika hospitali hiyo.

Katibu tawala wa wilaya ya Ubungo  ameiomba hospitali ya Aga khan kuanzisha huduma ya upasuaji kwa kina mama ili kurahisisha huduma kwa wakazi wa Ubungo kutokana na kutokuwepo kwa hospitali inayotoa huduma hiyo.

Amesema katika  manispaa hiyo hakuna hospitali ya karibu ya kufanya upasuaji wa uzazi hivyo ili.kuokoa maisha ya wakazi wanaohitaji huduma hiyo.

"Mkianzisha huduma ya upasuaji hasa upasuaji wa uzazi  itasaidia wananchi wa Ubungo wanaoishi maeneo ya ndani kuweza kupata huduma hiyo katika hospitali hii kwani katika wilaya ya Ubungo hakuna hospitali ya karibu inayotoa huduma ya Upasuaji kwa wakina mama na kusubabisha kupoteza maisha kwa kufuata huduma hiyo mbali" Amesema Mkumbo.

Aidha ameipongeza hospitali hiyo kuweza kujenga kituo hicho katika wilaya hiyo kwani wamesegeza huduma ya afya bora kwa wakazi wa Ubungo na kuwataka wananchi kufika kutibiwa katika hospitali hiyo kwani itatoa huduma kwa bei nafuu na rafiki kwa wakazi wote.

Amesema wananchi na wakazi wa Kimara wanapaswa kufika kupata huduma katika kituo hicho na kuacha kufikiri kuwa ni hospitali ya watu wa kipato cha juu ,lakini ni kwa watu wote na wa vipato vyote kwani itatoa huduma bora na nafuu kwa kila mmoja.

Kwa upande wake Dr.Omary Sherman (Head of Pathology AKHST)amesema wakazi wa Kimara wafike kutibiwa katika kituo hicho kwani kitatoa huduma kwa bei nafuu na rafiki kwa kila mmoja .

Naye Mkurugenzi mkuu wa Magonjwa ya Moyo Dr.Mustapha kapumi amesema wanatarajia kujenga vituo kila sehemu ili kusogeza huduma karibu na wananchi na kusema kwa sasa wameshajenga vituo 12 ,ambapo amewataka wakazi wa Kimara kutuma na kutunza kituo hicho.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages