Na Heri Shaaban
MKUU wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema, amewataka Wafanyakazi wa Shirika la umeme Tanzania TANESCO kupiga vita rushwa sehemu ya kazi.
Sophia Mjema aliyasema hayo Dar es SaPwani Jana, wakati wa uzinduzi wa mfuko wa WANAWAKE wa TANESCO kanda ya Dar es salaam na Pwani.
" WANAWAKE wenzangu wa shirika la umeme nimefarijika kwa kuunda JUKWAA la WANAWAKE muweze kupata fursa mbalimbali kupitia shirika lenu , Pia nawaomba mpige vita suala la rushwa sitaki nisikie katika Wilaya yangu ni Adui mkubwa" alisema Mjema.
Alisema pia alitaka Jukwaa hilo la TANESCO kujiwekea malengo na mikakati mbalimbali ikiwemo wabebe jukumu la kukamata vishoka wa shirika hilo
Alisema kufikia Tanzania ya Viwanda sio kazi ndogo hivyo akuna budi kushirikiana na Serikali katika kukuza MAENDELEO tuweze kufikia hatua hiyo.
Aliiomba JUKWAA la WANAWAKE Kanda ya Dar es Salaam na Pwani
Kuwa kitu kimoja katika kupanga maamuzi itafikia wakati shirika hilo linaongozwa na WANAWAKE .
Aliwaomba shirika hilo waache tabia ya kukata umeme ifikie wakati malengo ya Serikali inataka kila mtu alipe anavyoyumia bila fujo.
Akizungumzia JUKWAA alisema lilianzishwa mwaka Jana. Makamu wa Rais katika MKOA wa Dar es Salam majukwaa yote yanayoanzishwa washakuwa wajumbe wa MKOA.
Aidha aliwataka waheshimu taratibu za kazi kufanya kazi kwa bidii na kuwa waadilifu.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Tanesco wa JUKWAA la WANAWAKE Rukia Waandwi alisema Maadhimisho ya siku ya WANAWAKE Dunia yametengwa maalum kwa ajili ya kuwaenzi WANAWAKE ambao Daima wanapenda haki katika kuchapa kazi kwa bidii na maarifa...
Rukia alizungumzia umuhimu wa siku hiyo iliyotokana na WANAWAKE zaidi ya 200 waliofariki Mjini Newyork marekani kwa kukataa uonevu na dhuluma.
" WANAWAKE Hawa walikuwa wanafanya kazi katika kiwanda kimoja WAPO cha nguo nchini marekani ili ni funzo kuwa ulimwengu upaswa kuwathamini wanawake" alisema Rukia.
Alisem wanapinga kwa kuhudi zote WANAWAKE wavivu .Watoto kazini na wanaotumia vitendea kazi vibaya." Alisema
Alisema mwanamke MWALIMU wa kwanza katika ngazi familia hivyo inatakiwa kuwa mfano bora katika Jamii inayotuzunguuka.
" Malengo ya JUKWAA letu katika kusaidia Jamii kutoa misaada mbalimbali na tumeazimia kwa pamoja kukatwa mishahara yetu sisi WANAWAKE kwa ajili ya kuisaidia Serikali fedha hizo zijenge madarasa ya Shule ya msingi na sekondari"alisema
Mfuko huo wa JUKWAA la WANAWAKE uliyozinduliwa zilipatika jumla ya sh, milioni 9 haadi na cash sh, laki sita.
No comments:
Post a Comment