A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Sunday, March 25, 2018

Dk Tulia :Aongoza matembezi ya siku ya USONJI








Mkurugenzi wa Shule za Al Muntazir Mahmood Ladak(kushoto akizungumza na waandishi wa habari.

Naibu Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Tulia Akson ameotoa wito kwa shule zote nchini hususani shule binafsi kujikita kusaidia watoto wenye uhitaji maalumu,kwa lengo la kuwawezesha kupata elimu jumuishi ili kuwafanya wajione sawa na watoto wengine na wenye umuhimu katika jamii.

Hayo yamesemwa leo na  Naibu Spika wa Bunge katika matembezi ya siku ya Usonji Duniani  yaliyoandaliwa na Shule ya Al Muntazir jijini Dar es Salaam, na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali  wa Serikali wakiwemo wabunge ,yaliyobebaba kauli mbiu isemayo "TUWAPENDE  NA TUWALIDE".

Aidha Dr, Tulia amesema watoto wenye uhitaji maalumu wana haki sawa na wengine hivyo amezitaka shule binafsi kuweza kutoa mafunzo hayo kwa watoto wenye uhitaji maalumu kama inavyofanywa na Shule  za Al Muntazir kwani itasaidia kuelimisha jamii kuhusu Usonji,(Autism) pamoja na kuwawezesha kuona kuwa watoto hawa wana haki ya kupata elimu na kuthaminiwa kama wengine.

" Jamii inapaswa kuwajali , kuwapenda na kuwalinda watoto wenye uhitaji maalumu  wanauwezo wa kuelewa na kufanya vizuri darasani hata katika kazi mbalimbali kama kuchora kupaka rangi na wakifundishwa wanaweza hivyo jamii inapaswa kuwaona  ni watoto wenye umuhimu kwa jamii hivyo wakiwezeshwa wanaweza kufanya zaidi"amesema

Aidha  Naibu Spika amewashauri  viongozi wa  Shule za Al Muntazir kujenga mabweni ya kuwawezesha watoto hao kupata sehemu ya malazi ili kuwawezesha watoto wenye uhitaji maalumu kutoka katika maeneo  ya mbali kupata sehemu ya kulala,vilevile amezitaka Taasisi mbalimbali kujitokeza kutoa michango yao ili kuwawezesha watoto hao wasiokuwa na uwezo wa kuchangia gharama waweze kupata fursa ya elimu.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dr. Faustin Ndungulile ameishukuru shule hiyo kwa kuanzisha kitengo  cha watoto maalumu na kuona umuhimu wa watoto hao kuwa wana haki ya kupata elimu kama wengine hivyo ameahidi Serikali itashirikiana kikamilifu endapo watahitajika.

Naye Mkurugenzi wa Shule za Al Muntazir Mahmood Ladak amewashukuru viongozi wa seikali pamoja na wazazi waliojitokeza katika matembezi hayo, na kusema lengo la matembezi hayo ilikuwa ni kuielimisha jamii kuhusu Usonji (AUTISM),na kuwapenda kuwathamini watoto wenye uhitaji maalumu,kwani wana haki ya kupata elimu kama watoto wengine.

Hatahivyo amewata wazazi kuacha tabia ya kuwaweka watoto wenye Usonji (AUTISM) nyumbani  na kuamini kuwa hawawezi na badala yake kuwapeleka shule na kuwapa haki ya kupata elimu.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages