A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Wednesday, March 28, 2018

BANCABC yatangaza punguzo la riba za mikopo

BANCABC ambayo ni sehemu ya Atlas Mara iliyosajiliwa katika soko la Hisa London imepiga hatua kwa mara nyingine katika soko nchini kwa kutangaza punguzo katika tozo za mikopo ili kutoa uhueni kwa wateja wake wakati wa ulipaji wa mikopo na kuwawezesha wateja wapya kukopa kuanzia Aprili Mosi Mwaka huu.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa BancABC, Dana Botha alisema watapunguza riba kwenye mikopo ya masharti, huduma ya ‘over draft’ na mikopo ya nyumba kwa wateja wao.

“Mwaka jana benki nyingi zilipita katika wakati mgumu wa ukwasi,hivyo kufanya uwezo wa kukopesha kuwa mdogo.Kwa miezi kadhaa sasa serikali kupitia benki kuu ya Tanzania-BOT imekuwa ikisisitiza kuhusu punguzo la riba hili kwa kusaidia kupunguza masharti kama vile kiwango cha chini cha fedha kwa mabenki,viwango vya punguzo hati fungani za hazina na kukopesha mabenki kwa viwango vya chini.

“Hili limewezesha ukopeshaji kwa watu binafsi na makampuni mbalimbali ili kuimarisha biashara zao na hatimaye kuboresha uchumi na tunajivunia kuwa kati ya benki za kwanza kutangaza wazi kuhusu punguzo hili,” alisema.

Kwa mujibu wa Dana alisema kuwa hatua hizo mpya za serikali zitachochea ukuaji wa uchumi na benki nyingi zitaweza kukopesha na siyo kuwekeza katika hati fungani za hazina na serikali,hili litachochea wateja kukopa zaidi.

Naye Mkurugenzi wa Kitengo cha wateja binafsi na Wafanyabiashara wa BancABC, Joyce Malai alisema benki yao inahudumia zaidi ya wateja 60,000 ambao wanamiliki bidhaa tofauti za kibenki, hivyo fursa hiyo itawawezesha kuwashawishi wateja wao kupata bidhaa zaidi ya moja hasa mikopo ya nyumba ambayo ilikuwa changamoto kubwa hasa kwa wananchi wa daraja la kati na chini.

“Tutatumia fursa hii pia kuimarisha wafanyabiashara wetu wote na makampuni mbalimbali kupata mikopo nafuu na huduma ya ‘overdraft’ kutoka moja ya Benki bora ya kifedha nchini,” alisema.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages