MFANYABISHARA Timotheo Wandiba amehukumiwa kifungo cha miaka 81
jela baada ya kupatikana na hatia katika mashtaka 27 yaliyokuwa
yakimkabili ya kujipatia Sh.bilioni 2.1 kwa njia udanganyifu.
Aidha, Mahakama hiyo imewaachia huru washtakiwa Dickson Okololo na Simon
Efrem waliokuwa wakishtakiwa na Wandiba baada ya upande wa mashtaka
kushindwa kuthibitisha mashtaka dhidi yao pasipo kuacha shaka.
Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Mkuu Wilbard Mashauri, kwa niaba ya
Hakimu Joyce Minde aliyeandika hukumu hiyo, amesema upande wa mashtaka
kupitia mashahidi 14 imethibitisha makosa yote 82, kuwa mshtakiwa
alitenda kosa.
Katika makosa hayo 82, mashtaka 27 ni ya kughushi, 27 ya kutoa nyaraka
za uongo, 27 ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na Moja la
utakatishaji fedha.
Hakimu Mashauri amesema Mahakama hiyo imemtia hatiani mshtakiwa Wandiba
katika makosa 27 ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, baada ya
kuridhishwa na ushahidi uliotolewa na mashahidi wa upande wa mashtaka.
Hakimu Mashauri amesema katika makosa hayo 27, katika kila kosa
mshtakiwa Wandiba atatumikia kifungo cha miaka 3 jela, mbapo jumla
itakuwa ni miaka 81, lakini vifungo hivyo vitaenda kwa pamoja, hivyo
atatumikia kifungo cha miaka mitatu tu gerezani.
Aidha Hakimu Mashauri amesema Mahakama hiyo imewaachia huru washtakiwa
Okololo na Efrem katika makosa mengine yote baada ya upande wa mashtaka
kushindwa kuyathibitisha pasipo kuacha shaka yoyote.
Katika shtaka la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu ambalo limemtia
hatiani Wandiba, inadaiwa kati ya Desemba 3, mwaka 2012 na Februari
5,mwaka 2013, Dar es Salaam mshtakiwa alijipatia Sh.119,039,398.96
kutoka Benki ya Africa (BoA) kwa njia ya udanganyifu.
Pia wanadaiwa kughushi fomu za makubaliano ya kuhamisha fedha kutoka
Benki ya BOA ikionyesha akaunti ya Sogea Sauthom imeiomba benki hiyo
kuilipa akaunti ya Tracom Sh 2,119,039,398.96.
Katika shtaka la utakatishaji fedha, inadaiwa walilitenda kati ya
Desemba 4, 2012 na Aprili 30, mwaka 2014 walijipatia Sh.2,119,039,398.96
kutoka akaunti ya Sogea Sauthom katika benki ya (BoA) kwenda akaunti ya
Tracom NMB tawi la Ban House wakati wakijua fedha hizo ni zao la
uhalifu la kosa la kughushi.
Hata hivyo, upande wa mashtaka umesema haujaridhishwa na uamuzi uliotolewa na mahakama na watakata rufaa.
Post Top Ad
Your Ad Spot
Tuesday, March 13, 2018
Ahukumiwa Kwenda Jela Miaka 81
Tags
KITAIFA#
Share This
About kilole mzee
KITAIFA
Labels:
KITAIFA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment