A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Saturday, February 3, 2018

DIWANI WA KATA YA SALANGA ABORESHA MIUNDO MBINU YA BARABARA.


Diwani wa kata ya Salanga jijini Dar es salaam Harun Mdoe amekuwa na mpango mkakati wa mda mfupi na mrefu kuhusiana na barabara ambayo kwa sasa imekua kero kwa wananchi wa eneo hilo.

Mdoe amesema hayo leo alipotembelea barabara hiyo ambayo inaunganisha Matangini, Michungwani, King'ongo, Matosa, Kata ya Goba pia kuelekea Bagamoyo ambapo kwa mkakati wa mda mfupi wamekuwa wakiweka vifusi ambavyo vinasaidia angalau kupitika kwa urahisi.




Kutokana na kero hiyo pia amewataka wananchi wanaoishi maeneo hayo kuacha mara moja tabia ya kumwaga maji barabarani ambayo yanasababisha uharibifu na wataoendelea kufanya hivyo watachukuliwa hatua za sheria.

Kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa wa Michungwani Ismaili Kipungula amesema kuwa kuna shida kubwa katika barabara hiyo ambayo inaunganisha mitaa mitatu.




"hii barabara imekuwa ni tatizo kwamba imeoza na sio kuharibika tumejaribu kuhangaika kama mtaa tukishirikiana na wananchi pamoja  Diwani wetu kama mnavyoona hizi ni jitihada za wananchi wenyewe lakini barabara bado sio nzuri hivyo tunaiomba Serikali waiangalie hii barabara pia wenzetu wa Tarura ambao wamekubali kutengeza wafanya haraka kwani ilifika hatua tulika mawasiliano" amesema Kipungula

Aidha kwa upanda wake mkazi na mtumiaji wa barabara hiyo Upendo Mbise amesema kuwa kina mama wamekuwa wakijifungulia njiani kutokana na adha na ubovu ulipo mimi mwenyewe nikiwa kama shahidi juzi mama mmoja alijifungulia njiani hali ambayo ni hatari pia inaweza kupelekea hata kifo


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages