A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Saturday, February 3, 2018

KAMPUNI YA SIMU YA TECNO WAMETOA RASMI SIMU MPYA AINA YA CAMON CM

Kampuni ya simu za mikononi ikiwa chini ya kampuni mama ya TRANSSION HOLDINGS iliyopo China, imeachilia rasmi simu janja “smartphone” mpya yenye kioo kamili/enea au kwa lugha ya kiingereza (Full DISPLAY) yenye ukubwa wa uwiano “ratio” 18:9. TECNO CAMON CM ni simu mpya kabisa kwa mwaka 2018 . 

Mambo mengi yanatarajiwa na wadau kutoka katika simu hii mpya “CAMON CM” kwani ni muendelezo wa toleo lililopita la CAMON.

CAMON CM inabeba sifa kuu kubwa ambayo ni kua na kioo enea/kamili “FULL DISPLAY” chenye uwiano wa 18:9, kuifanya simu hii kua ya kwanza kutoka TECNO ambayo kioo chake hakina mipaka au mikato kulinganisha na simu zingine zenye ukubwa wa 16:9.
 Pia simu ina urefu wa nchi 5’7 ambayo itamuwezesha mtumiaji kutazama video, kucheza michezo “Games”, kuperuzi mitandao kwa raha zaidi kulinganisha na simu ambazo zina mipaka.

  
Camon CM inamonekano wa kifahari na umbo jembamba lenye ukubwa wa  7.75 mm.
Vigezo vingine ambavyo vinapatikana kwenye CAMON CM ni pamoja na kamera bomba yenye uwezo wa 13MP kamera ya mbele na nyuma,4G LTE, RAM 2GB, ROM 16GB, na betri yenye ukubwa wa  3000 mAh (Isiyotoka).

Simu hii ina rangi tatu ambazo ni “CITY BLUE”, MIDNIGHT BLACK na “CHAMPAGNE GOLD
  
CAMON CM sasa inapatikana,kwa taarifa zaidi tembelea http//www.tecno-mobile.com/tz

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages