Mkurugenzi
wa halmashauri ya wilaya Ileje Haji Mnasi akifanya kazi kwa vitendo
alivyokuwa anafanya ziara ya kukagua miradi ya ujenzi wa madarasa katika
shule ya msingi Izuba na shule ya msingi Ilulu na kuhakikisha wananchi
wanachangia nguvu zao kuleta maendeleo kwenye vijiji vyao
Mkurugenzi
wa halmashauri ya wilaya Ileje Haji Mnasi akifanya kazi kwa vitendo
alivyokuwa anafanya ziara ya kukagua miradi ya ujenzi wa madarasa katika
shule ya msingi Izuba na shule ya msingi Ilulu
Mkurugenzi
wa halmashauri ya wilaya Ileje Haji Mnasi akibadilisha mawazo na baadhi
ya viongozi walikuwa kwenye eneo la ujenzi wa madarasa katika shule ya
msingi Izuba na shule ya msingi Ilulu
HALMASHAURI
ya wilaya ya Ileje mkoani songwe imetumia zaidi ya shilingi milioni mia
moja themanini katika ujenzi wa madarasa kwa kutumia fedha za EPFR
ambazo hutolewa na serikali kwa ajili ya kuboresha sekta ya elimu kwa
shule za msingi.
Akizungumza
na waandishi wa habari wakati wa kukagua miradi hiyo,mkurugenzi wa
Ileje Haji Mnasi alisema kuwa jukumu la uongozi ni kuhakikisha kuwa pesa
inayotolewa na serikali inatumika kama ilivyokusudiwa na serikali kuu
kwa faida ya sekta ya elimu.
“Serikali
inatoa pesa nyingi sana hivyo tusipo simamia vizuri pesa hizi zitapotea
kitu ambacho Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe
Maguli hataki kabisa kusikia kuna pesa ambayo haitumiki kama
ilivyokusudiwa ndio maana nimeamua kuanza kukagua miradi yote ambayo
inatekelezwa katika halmashauri yetu” alisema Mnasi
Mnasi
aliwaomba wananchi kuchangia nguvu zao kuhakikisha shughuli za ujenzi wa
madarasa na vituo vya afya wanajitolea vilivyo ili kuendelea kufanya
kazi sambamba na kasi ya serikali ya awamu ya tano.“Mimi
binafsi nawaomba wananchi wajitolee kufyatua tofali ,kuchota
maji,kubeba mchanga na kusomba tofali ambazo zinakuwa zimenunuliwa na
serikali kwa ajili ya ujenzi ambao utakuwa na faida kwao na vizazi
vijavyo” alisema Mnasi
Aidha
Mnasi aliwapongeza wananchi wa halmashuri ya Ileje kwa kuendelea
kujitolea kufanya kazi kwa kuunga mkono juhudi zinazofanywa na serikali
ya wamu ya tano ambayo imelenga kuleta maendeleo kwa wananchi wake
“Mpaka
sasa kuna asilimia kubwa ambayo wananchi wamekuwa wakijitolea kufanya
kazi za kimaendeleo ambazo zinawahusu japo sio kwa asilimia kubwa
kutokana na idadi kubwa ya wananchi wanaoishi katika wialya hii hivyo
nitoe wito kwa wananchi kuendelea kujitokeza kwenye maendeleo ili
kuijenga ileje yetu mpya” alisema Mnasi
Mnasi
alisema kuwa kipaumbele cha halmashauri kwa sasa ni kuhakikisha kuwa
wanaboresha sekta ya elimu na sekta ya afya ili kukuza maendeleo ya
wilaya kwa kasi kubwa.“Ujenzi
unaendelea ni wa madarasa ya shule ya msingi Izuba na shule ya msingi
Ilulu na kuhakikisha wananchi wanachangia nguvu zao kuleta maendeleo
kwenye vijiji vyao” alisema Mnasi
Naomba
nimalizie kwa kupongeza serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Maguli kwa kufanya
kazi kubwa ya kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo kwa kuboresha
sekta za elimu,miundombinu afya na n.k
No comments:
Post a Comment