A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Wednesday, January 31, 2018

Wanamitindo waungana na Kasi ya Rais Magufuli, Mustafa Hasanali afunguka haya,Soma Hapa Zaidi


Wanamitindo waungana na Kasi ya Rais Magufuli, Mustafa Hasanali afunguka haya,Soma Hapa Zaidi
DAR ES SALAAM.
Wanamitindo wa Tanzania wameungana pamoja katika kuanzisha chama cha mitindo Tanzania (FAT) kinacholenga kuendeleza maslahi ya sekta ya mitindo kwa kuwaunganisha na kugawana ujuzi, uzoefu na rasilimali za sekta hiyo.

Viongozi wa Chama cha wanamitindo wakizindua Rasmi Chama hicho.

Chama hicho ambacho kimezinduliwa Leo jijini Dar es salaam kinatarajia kukuza sekta ya mitindo ya Tanzania kwa kushirikiana na wadau husika.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mwanzilishi wa Chama cha Mitindo Tanzania Mustafa Hassanali amesema kuwa chama hicho (FAT) kinatarajiwa kuwa chenye nguvu na taaluma ya uwezo wa kukuza na kuimarisha sekta ya mitindo nchini.
" Sisi kama wabunifu tunaunga mkono juhudi za Raisi wetu  John Pombe Magufuli katika kuifanya nchi yetu kuwa katika uchumi wa viwanda wa kati ifikapo 2025 kwa kuongoza katika bidhaa za nguo na vitambaa zinazotoka Tanzania" amesema Hassanali.

Ameongeza kuwa sekta ya mitindo Tanzania inakuwa kwa haraka sana, japo wadau wake wanakumbana na changamoto nyingi sana.

"Bado tuna uhakika wakati wa mafanikio umefika kupitia kuanzishwa kwa chama hiki chenye nia ya kuimarisha uhusiano nzuri wa wafanyaji kazi wa mitindo, wadau na katika ngazi ya serikali nchini Tanzania" amesema Hassanali.

Kwa upande wake mmoja wa waanzilishi wa chama hicho, Asia Idarous amesema chama hicho akijaanzishwa kwa ajili ya wabunifu tu, bali kwa wadau wote wa sekta ya mitindo ambapo inajumuisha majukwaa mbalimbali ya mitindo, taasisi za mitindo.

Huku wengine wakiwa wanamitindo  wa kuonyesha mavazi, wanamitindo wanaopanga muonekana wa mavazi, wapiga picha za mitindo, makampuni ya nguo, wazalishaji na wauzaji wa mavazi na wengine wengi wanaojiusisha na kazi za mitindo.

Amesema nchi nyingi duniani zilizoendelea katika sekta ya mitindo ni zile zilizofanya juhudi ya kuunda chama ambacho kitasimamia maslahi yao.

Naye Katibu mtendaji wa Balaza LA Sanaa Tanzania (BASATA) Godfrey Mngereza amewapongeza kwa hatua hiyo kwani chama hicho kitawasaidia kiujumla katika kupanga maamuzi na kushughulikia mambo yote yanayohusiana na wanachama wake.

Amesema kuwa uzinduzi huo umetokana na wanachama kwa lengo la kuendeleza ukuaji wa tasnia ya mitindo na kwa maendeleo ya Taifa kiujumla.

" Pale tunaposema Tanzania ya viwanda hatuwezi kuwasahau wabunifu ni watu wa msingi kwani ndio wanaokuja kutumika kwenye viwanda vya ngozi, mazulia pamoja na viatu" amesema Mngereza.

Aidha wafanyabiashara katika sekta ya mitindo nchini wanahimizwa kujiunga katika chama hiki kwaajili ya kupaza sauti zao kwa fursa mpya mitindo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages