Kuelekea msimu wa sikukuu maduka ya GSM
wanakuletea ofa maalum itakayowawezesha wateja wake kushinda safari ya
kuelekea Disney, Hong Kong nchini China.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam
Meneja Masoko wa Kampuni ya GSM Farida Rubanza ameeleza kuwa mteja
akifanya manunuzi yatakayofikia kiasi cha shilingi laki moja na nusu
(150,000) ataingizwa katika droo maalum itakoyomuwezesha kushinda safari
ya kuelekea Disney, Hong Kong China.
"Endapo mteja wetu atafanya manunuzi ya
kuanzia laki na nusu atafanikiwa kuingia katika droo maalum ambapo
mwanzo mwa mwezi January atangazwa mshindi ambaye atapata fursa ya
kusafiri Disney, Hong Kong, China" Alisema Farida.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa GSM
Foundation Fahad Ahmad amesema kuwa GSM wataendelea kutoa ofa kwa wateja
wao kupitia maduka yao mbalimbali jijini Dar es Salaam huku akisisitiza
bidhaa ni bora na gharama yake ni nafuu kulingana na maisha ya
mtanzania wa kawaida.
Meneja Mwendeshaji wa kampuni hiyo Yahya Zuhidi akizungumza na waandishi wa habari katika hafla hiyo
Picha zote na Brian Peter
No comments:
Post a Comment