Desemba 2017, Dar es Salaam na London: Huduma ya kuhamisha fedha
kidigitali inayoongoza WorldRemit na Kampuni ya kidigitali Tigo Tanzania
wameshuhudia ukuaji wa kasi wa huduma za kuhamisha fedha kwenda katika
akaunti za fedha za simu za mkononi nchini Tanzania, taarifa
zimebainisha.
Katika kipindi cha miaka miwili cha ushirikiano baina ya kampuni hizi,
huduma ya Tigo imebainika kuwa ndiyo huduma ya kutuma fedha inayokuwa
kwa kasi zaidi miongoni mwa washirika wa WorldRemit.
Huduma hii inawawezesha Watanzania katika zaidi ya nchi 50 kutuma fedha
kwenda katika akaunti za fedha za simu za mikononi kwa haraka. Wamiliki
wa akaunti za fedha za simu za mkononi pia wanakuwa na uwezo wa kutuma
fedha ndani ya nchi, kununua muda wa maongezi, kulipia ankara au kutoa
fedha taslimu kupitia mtandao mkubwa wa mawakala wa Tigo.
Licha ya Tanzania kutajwa kuwa ni moja ya nchi ambayo
ina gharama kubwa sana kutuma fedha miongoni mwa nchi za Afrika, huduma
hii maarufu inapunguza gharama za utumaji wa fedha wakati huohuo
ikifanya mchakato wa kutuma fedha kuwa wa haraka na salama zaidi.
Upokeaji wa fedha unachukua nafasi muhimu katika uchumi wa Tanzania.
Mwaka 2015 nchi ilipokea zaidi ya dola milioni 400 fedha kutoka nje ya
nchi, kwa mujibu wa Benki ya Dunia.
WorldRemit ni mfumo wa kidigitali wa kwanza unaotumia simu za mikononi
kutuma fedha unaowaruhusu wahamiaji wanaofanya kazi nje ya nchi kutuma
fedha kwa kufuata hatua chache moja kwa moja katika simu zao za mkononi
bila kutembelea au kusimama katika foleni kwa mawakala. Kampuni
inawajibika kwa 74% ya fedha zote zinazotumwa kupitia mfumo wa kutuma
fedha kimataifa kwenda katika huduma za fedha za simu za mikononi.
Andrew Stewart, Mkuu wa Kanda ya Mashariki ya Kati na Afrika kutoka
WorldRemit, alitoa maoni yake na kusema: “Ushirikiano wetu na Tigo
unatoa nafasi zaidi kwa mamlilioni ya watanzania wanaoishi na kufanya
kazi nje ya nchi kuwa na mbinu mbadala ambayo ni rahisi na salama ya
kuwasaidia marafiki na familia zao pasipo kupanga foleni kwa mawakala wa
kutuma fedha.”
“Mtanzania aliyehamia London, Stockholm au Sydney sasa anaweza kutuma
fedha kuja nyumbani kwa haraka na kwa urahisi – ikiwa inasaidia
kuhamisha fedha kwa haraka, usalama na uhakika zaidi kushinda mifumo ya
kutuma fedha isiotumia mtandao wa simu inayotegemea mawakala wa kutuma
fedha.”
Hussein Sayed, Afisa Mkuu wa Huduma za Kifedha za Simu za Mkononi wa
Kampuni ya Tigo Tanzania, aliongezea: “Tigo tumejizatiti katika kutoa
huduma kamili ya kifedha kwa wateja wetu. Kama sehemu ya malengo yetu ya
kuhakikisha upatikanaji wa huduma za kifedha, tunatazamia kuhudumia sio
tu soko la ndani ya mipaka ya Tanzania bali pia kwa watanzania wote
walioko nje ya nchi. Pamoja na hayo tunachukua hatua zote kuwapatia
wateja wetu mfumo wa uhakika na salama kwa ajili ya kutuma fedha
kimataifa.”
Kwa sasa wateja wa WorldRemit duniani kote wanafanya miamala 750,000 ya
kuhamisha fedha kila mwezi kutoka katika zaidi ya nchi 50 kwenda kwa
zaidi ya nchi wapokeaji 148.
Tembelea tovuti ya WorldRemit kwa taarifa zaidi kuhusu jinsi ya kutuma fedha Tanzania.
No comments:
Post a Comment