A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Tuesday, December 12, 2017

RAIS WA SOS CHILDREN’S VILLAGE AAHIDI KUIMARISHA USHIRIKIANO NA TANZANIA UTOAJI WA HUDUMA KWA WATOTO

Rais wa SOS Children’s Village Siddhartha Kaul, akiwa amembeba moja ya watoto wanaolelewa katika kituo cha SOS Children’s village kilichopo Ubungo wakati wa ziara yake hivi karibuni jijini Dar es salaam. Rais wa Shirika hilo alitua nchini kwa ziara ya siku 4 ambapo alikagua miradi ya shirika hilo na kufanya mazungumzo na viongozi wa Serikali.
Rais huyo akisalimiana na wamama wanaowalea watoto hao
Watoto wakitumbuiza wakati wa hafla hiyo
Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini wa SOS Children’s village Tanzania, Dk.Mary Nagu akizungumza wakati wa hafla ya kumkaribisha Rais wa Shirika hilo aliyetua nchini mwishoni mwa juma jijini Dar es salaam. 

Rais wa SOS Children’s Village, Siddhartha Kaul amesema taasisi hiyo itaendelea kuimarisha ushirikiano na serikali ya Tanzania ikiwa ni pamoja na kuendelea kusaidia miradi mbalimbali inayohusu kuwalinda watoto hapa nchini.
Akizungumza jijini Dar es Salaam mwishoni mwa juma katika ziara yake ya siku nne nchini Tanzania, alisisitiza kwamba kupitia SOS Children Village ataendelea kufanya kazi na Serikali ya Tanzania ili kuangazia masuala mbalimbali yanayoathiri usalama wa watoto nchini Tanzania.
“Tutaendelea kufanya kazi na jamii pamoja na serikali katika kuweka mazingira mazuri ya baadaye kwa watoto ili kuhakikisha huko mbeleni wanatimiziwa mahitaji yao muhimu,” alisema.
Ziara ya Rais huyo ilianzia Zanzibar ambako alitumia fursa hiyo kutembelea watoto na kukagua baadhi ya miradi ambayo inatekelezwa na asasi hiyo.
Kwa Dar es Salaam Kaul atakutana na watoto na kukagua miradi michache ambayo inasimamiwa na asasi hiyo pamoja na kubadilishana mawazo na viongozi mbalimbali wa Serikalini.
Kuhusu SOS Tanzania Bara na Zanzibar
SOS Children’s Villages Tanzania na Zanzibar ni asasi huru isiyo ya serikali na taasisi ya maendeleo ya jamii iliyosajiliwa Tanzania na Zanzibar inayohusiana na SOS Children’s Village International yenye makao makuu yake Innsbruck, Austria.
SOS Children’s Villages imelenga kufanya kazi za watoto ambao wamekosa malezi na wale ambao wapo kwenye hatari ya kukosa matunzo.
SOS inatoa malazi bora kwa kila mtoto. Tunawapa watoto hawa fursa kujenga uhusiano wa kudumu ndani ya familia na kuwasaidia kutengeneza maisha yao ya baadaye. Kwa sasa SOS CV TZ inafanya kazi zake Mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Mwanza, Iringa (Iringa Mjini na Mufindi), Zanzibar (unguja na Pemba)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages