Naibu Waziri wa Wizara ya Ofisi ya Makamu wa Rais Inayoshughulika na
muungano na Mazingira Mheshimiwa Kangi Lugola akizungumza na wananchi
ambao mashamba yao yameathirika kutoka na sumu ambayo imeeharibu mazao
yao pamoja na viumbe hai.
Moja
kati ya wakurugenzi wa Mgodi wa Nyarugusu Mine Co.Limited Fred Masanja
akionesha cheti NEMC ambacho naibu waziri alikikata.
Bwawa la kuhifadhia maji ya kemikali ambalo limeharibika na kusababisha maji mengi kuelekea kwenye shughuli za wananchi.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Ofisi ya Makamu wa Rais Inayoshughulika na muungano
na Mazingira Mheshimiwa Kangi Lugola ,akiwa na mwenyeji wake ambaye ni
Mkuu wa Wilaya ya Geita wakikagua eneo ambalo lilipasuka na kupeleka
maji ya sumu kwenye maeneo ya mashamba ya wananchi.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Ofisi ya Makamu wa Rais Inayoshughulika na muungano
na Mazingira Mheshimiwa Kangi Lugola akiangalia baadhi eneo ambalo
limepasuka.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Ofisi ya Makamu wa Rais Inayoshughulika na muungano
na Mazingira Mheshimiwa Kangi Lugola ,akitembelea na kuangalia miche ya
miti ambayo imekwisha kuathirika.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Ofisi ya Makamu wa Rais Inayoshughulika na muungano
na Mazingira Mheshimiwa Kangi Lugola ,akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Geita
Mwl Herman Kapufi na baadhi ya wananchi ambao wameathirika kutokana na
maji Hayo kwenye maeneo ya mashamba. (PICHA NA JOEL MADUKA)
Ekari
270 za mashamba ya wakulima kwenye kijiji cha Ziwani Kata ya Nyarugusu
Wilayani Geita zimeathiriwa na Sumu iliyotoka kwenye Bwawa la kuhifadhia
Kemikali lililopasuka kingo zake na maji kusambaa kwenye mashamba hayo.
Hali
hiyo imemlazimu Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano
na Mazingira Bw Kangi Lugola kuitaka kampuni ya Madini ya Nyarugusu
inayohusika na suala hilo kuwalipa fidia wananchi 57 ambao mazao yao
yameathirika.
Awali
Bw Lugola aliagiza muwekezaji huyo akamatwe kutokana na kile alichodai
kuwa ni uvunjifu wa sheria za utunzaji wa mazingira mgodini hapo na
kwamba uongozi wa mgodi huo ulimzuia Afisa Mazingira wa Wilaya ya Geita
Bi Hellen Eustace kutekeleza majukumu yake baada ya kufika mgodini hapo
kukagua namna wanavyozingatia utunzaji mazingira
Bw
Kangi alisema Mwekezaji haruhusiwi kuendelea na shughuli anazozifanya na
kufunga mgodi huo hadi watakapotekeleza mambo waliyoelekezwa
Mkurugenzi
wa Nyarugusu Mine Company Bw Fred Masanja amesema kusimamishwa kwa
shughuli zao kunaweza kuathiri ytendaji wao kwa kuwa Tani Laki moja na
20 hawataweza kuzizalisha na hivyo watapata hasara ya zaidi ya Sh
Milioni 600 hadi 700.
No comments:
Post a Comment