Watumishi wa Wizara ya Afya wakiongozwa na Mkurugenzi wa
kituo cha Lishe na Chakula Wizara ya Afya
Dkt. Vicent Assey (aliyevaa tisheti ya bluu) mapema leo katika matembezi
ya Siku ya Kisukari Duniani yaliyoanza chuo cha Muhimbili mpaka Viwanja vya
Mnazi mmoja.
Watumishi na Wadau
mbali mbali wa masuala ya Afya wakinyoosha viungo baada ya matembezi yaliyo
anzia Chuo cha Muhimbili na kukomea viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es
salaam katika maazimisho ya siku ya Kisukari Duniani huku kauli mbiu ikiwa ni Wanawake na Kisukari.
Kaimu Mkurugenzi wa Elimu ya Afya kwa Umma (HEU) Said Makora
(wakushoto) akimsikiliza Mkurugenzi
msaidizi wa NCD Wizara ya Afya Dkt. Sara Maongezi wakati wa maazimisho ya siku
ya Kisukari Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es
Salaam.
Mkurugenzi wa kituo cha Lishe na Chakula Wizara ya Afya Dkt. Vicent Assey akitoa neon mbele ya wadau
wa Afya na Ugonjwa wa Kisukari (Hawapo kwenye picha) wakati wa maazimisho ya
siku ya Kisukari Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini
Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Kinga
Dkt. Neema Rusibamayira ambae alimwakilisha mgeni rasmi Mh. Ummy Mwalimu
akisoma taarifa mbele ya wadau wa Afya na Kisukari nchini (hawapo kwenye picha)
katika maazimisho ya Siku ya Kisukari
Duniani ambayo kikomo chake ni Novemba 14. Wakwanza kushoto ni Dkt Waane na wa mwisho ni
Mkurugenzi msaidizi wa NCD Wizara ya Afya Dkt. Sara Maongezi.
Picha ya pamoja ikiongozwa na Mkurugenzi wa Kinga Dkt. Neema Rusibamayira katika maazimisho ya Siku ya Kisukari Duniani
yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.
NA WAMJW-DA ES SALAAM.
WATANZANIA
waaswa kujihusisha na tabia ya kupenda kufanya mazoezi ili kuepuka ugonjwa wa
kisukari na viashiria vyake katika jamii
yetu inayotuzunguka.
Hayo
yamesemwa na Mkurugenzi wa Kinga Wizara ya afya Dkt. Neema Rusibamayila
alipomwakilsha Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto Mhe.
Ummy Mwalimu wakati wa kuadhimisha siku
ya Kisukari duniani leo jijini Dar es salaam.
“Watanzania
tunatakiwa kupenda kujijengea tabia ya kufanya mazoezi mara kwa mara ili kuweza
kuepuka magonjwa yasioambukiza ikiwemo Kisukari na viashiria vyake kwa ujumla”
alisema Dkt. Rusibamayila.
Aidha
Dkt. Rusibamayila amesema kuwa
watanzania wengi hawana budi
kujikinga na ugonjwa huo kwani asilimia 60 wanafariki kwa ugonjwa huo duniani
kila mwaka.
Kwa
mujibu Wa Dkt. Rusibamayila amesema kuwa asilimia kubwa ya wanawake nchini wana
uzito mkubwa,mafuta mengi na hawajihusishi na mazoezi hivyo hupelekea kupata
hathari za ugonjwa wa kisukari.
Mbali
na hayo Dkt. Rusibamayila amesema kuwa
licha tu ya kufanya mazoezi lakini pia wanatakiwa kuepuka matumizi ya vileo
kama vile uvutaji tumbaku,unywaji pombe na uvutaji wa shisha ili kuepuka
magonjwa yasioambukiza kwani yamekuwa hatari kwa watanzania.
Kwa
upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha chakula na Lishe (TFNC) Dkt. Vicent
Assey amesema kuwa sambamba na kufanya mazoezi watanzania wanatakiwa kuzingatia
mlo ulio bora ili kuepuka ugonjwa wa kisukari.
Aidha
Dkt Assey amesisitiza walimu , wazazi na
watoa huduma ngazi ya jamaii wanatakiwa kuwa kipaumbele katika kuelimisha
watoto na jamii nzima kwa ujumla juu ya lishe bora ambayo huleta kinga zidi ya
kisukari.
Siku
ya kisukari Duniani huadhimshwa Novemba 14 kila mwaka na mwaka huu imeadhimishwa
sambamba na matembezi ya hiari na mazoezi ya pamoja kutoka viwanja vya
muhimbili mpka Mnazi mmoja na kubeba Kauli mbiu isemayo “MWANAMKE NA KISUKARI “
ikimaanisha wanawake wawe mstari wa mbele katika kupambana na ugonjwa huo.
No comments:
Post a Comment