Taasisi
ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Hospitali ya Saifee
ya Mjini Mumbai nchini India wamefanya upasuaji mkubwa wa moyo kwa
wagonjwa 15 katika kambi maalum ya upasuaji ya siku sita inayomalizika
kesho.
Upasuaji
wa moyo unaofanyika katika kambi hii ambayo imeanza Jumatatu tarehe
8/11/2017 hadi Jumamosi tarehe 11/11/2017 ni ya upasuaji wa kufungua
kifua kwa watu wazima. Upasuaji uliofanyika ni wa kupandikiza mishipa ya
damu kwenye moyo (CABG – Coronary Artery Bypass Grafting), na kubadili
milango miwili hadi mitatu ya moyo (Valve Replacement).
Kwa
mara ya kwanza hapa nchini tumefanya upasuaji wa kurekebisa mshipa
mkubwa unaotoa damu kwenye moyo kwenda sehemu zote za mwili (Aortic
Aneurysm Repair).
Tulifanya
upasuaji kwa wagonjwa watatu kwa siku, wote hawa wanaendelea vizuri na
wataruhusiwa pindi afya zao zitakapoimarika. Baadhi yao ambao
tumewafanyia upasuaji jana na juzi wako katika chumba cha uangalizi
maalum na wengine wako wodini wameshaanza kufanya mazoezi.
Kama
wagonjwa hawa wangeenda kutibiwa nje ya nchi Serikali ingelipia zaidi ya
milioni 405 kwani gharama za mgonjwa mmoja kwenda kutibiwa nje ya nchi
ni zaidi ya milioni 27. Gharama za matibabu haya hapa nchini kwa
wagonjwa 15 ni milioni 225 (milioni 15 kwa mgonjwa mmoja).
Changamoto
kubwa tunayokabiliana nayo katika matibabu ya wagonjwa wetu ni wagonjwa
wengi tunaowapokea mioyo yao kutokuwa katika hali nzuri. Tunawashauri
wananchi kujenga tabia ya kupima afya zao mara kwa mara hii itawasaidia
kujuwa kama wana matatizo ya moyo au la na hivyo kupata tiba kwa wakati.
Kama
mnavyofahamu matibabu ya moyo ni ya gharama hivyo basi tunaendelea
kuwahimiza wananchi kujiunga na mfuko wa taifa wa bima ya afya ambao
utawasaidia kulipa gharama za matibabu pindi watakapougua na kuhitaji
kupata matibabu.
Kwa
namna ya kipekee Taasisi inaishukuru Hospitali ya Seifee kutokana na
ushirikianao mzuri tuliokuwa nao, licha ya kutoa matibabu kwa wagonjwa
tumekuwa tukibadilishana ujuzi wa kazi wakati wa kufanya upasuaji. Kwa
mwaka huu hii ni mara ya pili kwa wataalamu hawa kuja katika Taasisi
yetu. Mwezi wa tatu mwishoni tulifanya nao kambi ya upasuaji wa kufungua
kifua kwa wagonjwa nane (8).
Aidha
tunatarajia kuwa na kambi maalum ya matibabu ya moyo ya bila kufungua
kifua kwa kutumia mtambo maalum wa Cathlab kwa watu wazima itakayoanza
tarehe 14/11/2017 hadi tarehe 19/11/2017. Katika kambi hii ambayo
tutashirikiana na wenzetu kutoka Taasisi ya Sharjah Charity kutoka Falme
za Kiarabu tunatarajia kufanya upasuaji wa moyo kwa wagonjwa 50.
Tunawaomba
wananchi waendeleee kuchangia damu kwani wagonjwa wanaofanyiwa upasuaji
wa moyo wanahitaji kuongezewa damu wakati wanapatiwa matibabu. Mgonjwa
mmoja anahitaji damu kati ya chupa 5 hadi 6.
Kwa
mtu mmoja mmoja au kikundi cha watu ambao wanapenda kuchangia damu
tunawaomba wafike Taasisi ya Moyo iliyopo Muhimbili mkabala na Maabara
kuu. Kwa maelezo zaidi wawasiliane kwa simu namba 022-2151379 au 0713304149.
Daktari
Bingwa wa Upasuaji wa Moyo na Mishipa ya Damu ambaye pia ni Kaimu
Mkurugenzi wa Idara ya Upasuaji kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
(JKCI) Bashir Nyangasa akiongea na waandishi wa Habari leo jijini Dar es
Salaam kuhusu kambi maalum ya upasuaji ambayo imefanywa na Taasisi hiyo
kwa kushirikiana na Hospitali ya Saifee ya Mjini Mumbai nchini India
ambapo wagonjwa 15 wamefanyiwa upasuaji. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa
Idara ya Uuguzi Roberth Mallya na kushoto ni Daktari bingwa wa usingizi
na wagonjwa mahututi Anjela Muhozya akifuatiwa na Daktari Bingwa wa
Upasuaji wa Moyo na Mishipa ya Damu kutoka Hospitali ya Saifee Ali Ascar
Beliranwalwa.
Daktari
Bingwa wa Upasuaji wa Moyo na Mishipa ya Damu ambaye pia ni Kaimu
Mkurugenzi wa Idara ya Upasuaji kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
(JKCI) Bashir Nyangasa akiongea na waandishi wa Habari leo jijini Dar es
Salaam kuhusu kambi maalum ya upasuaji ambayo imefanywa na Taasisi hiyo
kwa kushirikiana na Hospitali ya Saifee ya Mjini Mumbai nchini India
ambapo wagonjwa 15 wamefanyiwa upasuaji. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa
Idara ya Uuguzi Roberth Mallya na kushoto ni Daktari bingwa wa usingizi
na wagonjwa mahututi Anjela Muhozya akifuatiwa na Daktari Bingwa wa
Upasuaji wa Moyo na Mishipa ya Damu kutoka Hospitali ya Saifee Ali Ascar
Beliranwalwa.
Mkutano wa waandishi wa Habari ukiendelea kuhusu kambi maalum ya upasuaji ambayo imefanywa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Hospitali ya Saifee ya Mjini Mumbai nchini India ambapo wagonjwa 15 wamefanyiwa upasuaji. Upasuaji uliofanyika ni wa kupandikiza mishipa ya damu kwenye moyo (CABG – Coronary Artery Bypass Grafting), kubadili milango miwili hadi mitatu ya moyo
(Valve Replacement) na kurekebisha mshipa mkubwa unaotoa damu kwenye
moyo kwenda sehemu zote za mwili (Aortic Aneurysm Repair).
No comments:
Post a Comment