Mshtakiwa
Harbinder Singh Sethi,ameoimba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
kumruhusu kwenda kupatiwa matibabu ya puto lake lililoisha muda nchini
Afrika Kusini kwa daktari wake maalumu kwa madai ya kwamba Hospitali ya
Taifa ya Muhimbili wamemueleza kuwa hawawezi kufanya upasuaji huo.
Maombi
hayo yamewasilishwa mahakamani hapo na wakili wake, Joseph Sungwa leo
Novemba 10/2017 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi, wakati shauri
hilo linalomkabili Sethi na James Rugemarila lilipopelekwa kwa kutajwa
na Mawakili wa Serikali, Vitalis Peter na Leonard Swai kudai upelelezi
haujakamilika.
Katika
kesi hiyo, Sethi na James Burchard Rugemarila wanakabiliwa na mashtaka
12 ya uhujumu uchumi kwa kula njama, kujihusisha mtandao wa uhalifu ,
kighushi, kutoa nyaraka za kughushi, kujipatia fedha kwa njia za
udanganyifu, kutakatisha fedha na kuisababisha hasara ya USD 22,
198,544.60 na Sh 309,461,300,158.27.
Akiwasilisha
maombi hayo, wakili Sungwa alidai alielezwa na mteja wake kwamba baada
ya kufanyiwa vipimo na Muhimbili, walimweleza hawana ujuzi wa kumfanyia
upasuaji wa puto.hilo na endapo litaendelea kubaki mwilini mwake
linaweza kupasuka muda wowote na kuzalisha sumu ambayo litaatarisha
maisha yake na njia pekee iliyobakia ni kwa mshtakiwa Sethi kumuona
daktari wake anayeishi Afrika Kusini.
“Ili
mshtakiwa aweze kuja mahakamani kuudhuria kesi yake na hatimae kuweza
kujitetea, tunaomba kama inawezekana aende kumuona daktari wake ambaye
anaishi Afrika Kusini kwa matibabu”, alidai Sungwa.
Ombi
hilo lilipingwa vikali na wakili wa serikali,Swai akidai Muhimbili
haijashindwa kumfanyia upasuaji wa puto mshitakiwa huyo, bali
anajicheleweshwa mwenyewe kutokana na kutaka uwepo wa daktari wake wa
Afrika Kusini.
Swai
alidai kwa taarifa kutoka magereza ambako mshtakiwa ndiko anaishi imedai
repoti kutoka Muhimbili ilisema kuwa inaouwezo wa kumfanyia operesheni
mshtakiwa lakini mshtakiwa mwenyewe anahitaji daktari wake aliyeko
Afrika Kusini ndiye aje kumtibu.
“Tanzania
tunao madaktari jambo hili la kumleta daktari kutoka nje ya nchi
linahitaji kufuata taratibu na litahusisha taasisi za mbali mbali
ikiwemo serikali ili kumruhusu daktari wake aje nchini kumtibu” amedai
Swai.
Akielezea
juu ya upelelezi Swai alidai wapo katika hatua nzuri na wanataka kwenda
mahabusu kuchukua maelezo ya onyo ya washitakiwa na iwapo amri ikitoka
wachunguzi wataenda kuchukua maelezo yao.Hoja
ya upelelezi iliibuliwa na Wakili Michael Ngalo,aliyedai upelelezi
umechukua muda mrefu ni takriban miezi mitano saaa haujakamilika na
washitakiwa wapo mahabusu.
Baada
ya kusikiliza hoja za mawakili wa pande zote mbili, Hakimu Shaidi
alisema juu ya mshitakiwa kama anawezo wa kutibiwa Muhimbili ama la,
mahakama hiyo haina mamlaka ya kutoa amri yoyote hivyo wawasilishe
maombi Mahakama Kuu.
Kesi hiyo imeahihirishwa hadi Novemba 24, mwaka huu.
No comments:
Post a Comment