Hospitali
ya Aga Khan kwa kushirikiana na hospitali ya Taifa ya Muhimbili imeanza
kutoa huduma ya upasuaji kwa kuweka matiti bandia kwa wanawake
walioathirika na ugonjwa wa Saratani ya matiti.
Matiti
hayo yanatengenezwa kitaalamu kwa kumfanyia upasuaji muhusika ili
kurudisha matiti yake ingawa haitarudi katika hali yake ya kawaida kama
ilivyokuwa awali kabla ya kupata ugonjwa wa saratani ya matiti.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Daktari Bigwa wa
Upasuaji kutoka hospital ya Aga Khan Dk. Aidan Njau, amesema kuwa hatua
hiyo itawasaidia wakina mama ambao watakuwa wameathirika na ugonjwa wa
saratani ya matiti.
Amesema
hii ni mara ya kwanza kufanyika, hivyo na italeta hauweni kwa wagonjwa
kutokana na wakina mama waliokuwa wanajisikia vibaya baada ya kupata
ugonjwa wa saratani ya matiti.
“Tutaweza
kurudisha matiti ya kinamama ambayo yalitolewa kutokana na saratani,
hivyo itakuwa faraja kwao kwani watakuwa katika hali ya kawaida
kimuonekano kama ilivyokuwa awali kabla ya ugonjwa” amesema Dk Njau.
Hata
hivyo amefafanua kuwa elimu hiyo ya kitaalamu ya kufanya upasuaji wa
kurudisha matiti ya kinamama (matiti bandia) ameipata nchini Marekani
baada ya kwenda kusoma huko (Scholar ship).
Naye
Daktari Bigwa wa Upasuaji kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dk.
Edwin Malima zoezi hili linapaswa kuugwa mkono na watanzania wote.
Amesema
kutokana na hatua hiyo wameamua kuwapeleka wanafunzi wawili wa Chuo Cha
Muhimbili (MUHAS) katika hospitali ya Aga Khan kwa ajili ya kupata
elimu ya kufanya upasuaji wa kutengeneza matiti bandia ya kinamama.
“Wamekuja
kujifunza jinsi ya kufanya upasuaji wa kurudisha matiti ambayo
yalivunwa kutokana na ugonjwa wa saratani” amesema Dk. Malima.
No comments:
Post a Comment