Dar es Salaam. Mwenyekiti wa kampuni inayoshughulikia uwekezaji wa
mitaji na dhamana (Egma), Harry Kitilya na waliokuwa maofisa wa benki ya
Stanbic, Shose Sinare na Sioi Solomon bado wanaendelea kusota rumande
kutokana na upelelezi wa kesi inayowakabili bado haujakamilika.
Wakili
wa Serikali Mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi ameeleza mbele ya Hakimu
Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa leo Ijumaa kuwa upelelezi wa kesi hiyo
bado haujakamilika.
Soma: Wakili aomba kesi ya utakatishaji fedha dhidi ya akina Kitilya ifutwe
Pia
ameeleza kuwa bado wanasubiri awamu ya pili ya upelelezi kutoka nchini
Uingereza, kutokana na hilo ameomba kesi hiyo ipangiwe tarehe nyingine
kwa ajili ya kutajwa.
Baada ya ombi hilo Hakimu Mwambapa
ameahirisha kesi hiyo hadi Novemba 10, 2017 kwa ajili ya kutajwa ili
kuangalia kama upelelezi utakuwa umekamilika ama la.
Post Top Ad
Your Ad Spot
Friday, November 3, 2017
Home
Unlabelled
Kitilya na wenzake waendelea kusota rumande
Kitilya na wenzake waendelea kusota rumande
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment