WAZAZI
na Walezi wameaswa kuwasomesha watoto wa kike na kuachana na fikra
potofu kuwa kumsomesha mtoto wa kike ni kupoteza rasilimali fedha kwani
maisha ya sasa bila elimu ni changamoto kubwa kwa mtoto wa kike.
Kauli
hiyo imetolewa hivi karibuni na Kenneth Komba kutoka Idara ya Elimu mkoa
wa Iringa kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza wakati
alipokuwa mgeni rasmi wakati wa mahafali ya kumi kidato cha nne katika
shule ya Sekondari ya Wasichana ya Spring Valley iliyopo Mkoani Iringa.
Alisema
kuwa mtoto wa kike akipatiwa elimu kuna uwezekano mkubwa kwa taifa kuwa
na maendeleo kutokana na kuwajibika kwao katika maisha ya kila siku
hivyo wazazi na walezi ni muhimu kuwasomesha watoto wa kike kwa lengo la
kuendeleza ndoto walizonazo.
Alisema
kuwa jukumu la kusomesha elimu ya msingi hadi sekondari ni la serikali
lakini wazazi na walezi wanaosomesha shuleni hapo ni kuisaidia serikali
hivyo ipo tayari kupokea changomoto zote katika shule hiyo na
kushirikiana kuzitatua.
Komba
aliipongeza shule ya sekondari Spring Valley kwa kuwa moja ya shule
zinazofanya vizuri mkoani hapa kielimu na tabia kwani ni moja ya shule
ambazo idara ya elimu haipati malalamiko ya mara kwa mara kutoka shuleni
hapo.
Aidha
Komba aliwataka wahitimu hao kusoma mazingira ya maisha popote
watakapokuwa na kuamua namna ya kujiajiri ili mradi isiwe shughuli
zinazopingana na sheria na maadili ya kijamii, kama vile kuuza madawa ya
kulevya, ukahaba, unyang'anyi na mambo mengine yanayofanana na hayo
ambayo watajiingiza matatani na kuonekana wabaya.
Awali
mkuu wa shule ya Wasichana Spring Valley, Adia Mbwanji alisema kuwa
uongozi wa shule hiyo umeweka mikakati mbalimbali itakayotekelezwa mwaka
2018 ikiwemo ujenzi wa ukuta upande wa Kusini mwa shule, upanuzi wa
maktaba, ununuzi wa gari la shule na kukarabati mifumo ya maji taka na
maji safi.
Alisema
kuwa shule hiyo inayomilikiwa na kanisa la Baptist Convention of
Tanzania imejipanga kujenga chumba cha kompyuta na kununua komputa
zenyewe ili kutoa elimu hiyo kwa wanafunzi kuendana na ulimwengu wa
sayansi na teknolojia.
Kwa
upande wao wahitimu kwa kupitia msoma risala, Happy Njavike walisema
kuwa shule hiyo inatakiwa kuboresha ujenzi wa jengo la maabara vifaa
vyake vinunuliwe ili kutoa fursa kwa wanafunzi wengi kujifunza kwa
vitendo hasa masomo ya sayansi kwa lengo la kukuza ufaulu na kuongeza
ujuzi katika masomo ya sayansi.
Wanafunzi wa shule ya wasichana ya Spring valley wakicheza muziki katika sherehe za kumaliza kidato cha nne
wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana ya Springa Valley wakiwa katika picha ya pamoja
Baadhi
ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana ya Spring Valley
iliyoko katika manispaa ya Iringa wakiwa katika mafunzo ya vitendo
shuleni hapo
No comments:
Post a Comment