A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Monday, November 20, 2017

RC MAKONDA KWA HILI MUNGU ANAKUONA.

Mkuu wa Mkoa akitoa neno la shukrani kwa
Hii meli ni hospitali inayotembea sasa ipo Dar es Salaam kwaajili yakutoa huduma ya afya  bure kwa wakazi wa jiji hilo
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda akishikana mikono na mmoja wa maofisa wa jeshi la china.



Msanii wa filamu nchini Bongo muvi Jacob Stevene maarufu kama JB akipata matibabu ndani ya meli hiyo
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda, alie kaa kwenye kiti akiuliza jambo la kiutaalamu kuhusu meli hiyo kwa baadhi ya makampeni wa meli hiyo mara baada yakuwasili jijini hapa kwakutoa huduma ya afya na matibabu bure.


Meli kubwa ya Jeshi la Jamuhuri ya China yenye Hospital ndani imewasili Leo ikiwa na Madaktari Bingwa 381,Vifaa na Madawa ya kutosha kwaajili ya kuanza kwa zoezi la Upimaji na Matibabu Bure kwa wakazi wa Dar es Salaam.
 

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. PAUL MAKONDA ametembelea Meli hiyo na kujionea namna imesheheni Vifaa tiba vya Kisasa ambapo ndani yake vipo vyumba 8 vya Upasuaji, Vyumba vya ICU, Wodi za Wagonjwa, Vyumba vya Madaktari, Mitambo ya kisasa, Mahabara na Sehemu ya Wagonjwa kupumzika.
 

Meli hiyo ya kipekee ina Helicopter kwaajili ya wagonjwa ambapo kwa Ulimwenguni Meli za Aina hiyo zipo Mbili pekee ambapo moja ni hii iliyokuja Tanzania na nyingine ipo Nchini Marekani.

RC MAKONDA amesema Meli hiyo ina mfumo maalumu wa Mawasiliano Kati ya Meli na Taifa la China pale inapotokea Ugonjwa umeshindikana.



Tayari Jopo la wataalamu 30 wameenda Hospital za Amana, Temeke, Mwananyamala na Ocean Road kwaajili ya kukarabati na kufunga vifaa vipya kwa vile vitakavyobainika vilivyoharibika au Kufa.



Amesema *lengo la Serikali ni kuhakikisha Hakuna mwananchi anaepoteza maisha kwa kigezo cha kukosa huduma.



Amewasihi Wananchi wenye magonjwa yaliyoshindikana kwa muda mrefu kuchangamkia Fursa hii ya matibabu Bure chini ya Madaktari Bingwa kutoka China.



Kwa upande wake kiongozi Mkuu wa Meli hiyo Kamanda GUAN BAILIN amesema wamekuja na vifaa vya kutosha na madaktari waliobobea hivyo wananchi Wajitokeze kwa wingi.
ANGALIA FULL VIDIO HAPA 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages