Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mheshimiwa PAUL MAKONDA leo
amepokea zaidi ya Tani 405 za Nondo kutoka kiwanda cha AM Steel and Iron Mills
Ltd na Mifuko ya Saruji 500 kutoka Mfuko wa Hifadhi ya jamii wa LAPF kwaajili
ya Ujenzi wa Ofisi 402 za Walimu wa Shule za Msingi na Sekondari Dar es Salaam.
Nondo hizo zenye thamani ya zaidi ya Shillingi Million 150
zimetolewa kama utangulizi ambapo Kiwanda hicho kimesema kitatoa Nondo za kujenga
ofisi zote 402 za Walimu.
Akipokea Nondo hizo RC MAKONDA ameshukuru kiwanda hicho kwa
kuunga Mkono kampeni hiyo inayolenga kurejesha heshima kwa walimu na kuwapa
morali ya kufanya kazi ili kuleta matokeo chanya kwa Wanafunzi.
Wakati huohuo Mfuko wa hifadhi ya Jamii LAPF umemkabidhi RC
MAKONDA Kiasi cha Shillingi Million 5 kwaajili ya kununua Mifuko 500 ya Saruji
za Ujenzi wa Ofisi za Walimu.
RC MAKONDA amewahimiza Wananchi na wadau kuendelea kuchangia
kampeni ya ujenzi wa Ofis za walimu kupitia Saruji, Kokoto, Mchanga, Nondo Mbao,
Milango, Madirisha na Bati ili kufanikisha kampeni hiyo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kiwanda hicho Shekh SHAHID
SALIM amesema watatoa kiasi chote cha mahitaji ya Nondo zinazohitajika kwakuwa wanatambua
umuhimu wa Walimu na kazi kubwa anayoifanya RC MAKONDA kwenye Mkoa wa Dar es
Salaam.
Nae Meneja Masoko na Mawasiliano LAPF Bwana JAMES MLOWE
amesema kuwa wameamua kumuunga mkono RC MAKONDA kwakuwa fedha zinazotolewa
kwake zinafanya kazi iliyokusudiwa.
Tayari kasi ya ujenzi wa Ofisi za walimu inaendelea katika
Shule mbalimbali jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa kiwanda hicho wakiwa kazini
Makonda akizungumza na wafanyakazi wa kampuni hiyo
No comments:
Post a Comment