Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akishindana kucheza muziki na
watoto wenye ualbino katika kituo cha Buhangija wakati wa hafla ya kula
chakula cha pamoja kilichoandaliwa na Kampuni ya Ulinzi Cyvalo Tanzania
Limited-Picha na Marco Maduhu - Malunde1 blog
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro ameshiriki katika hafla fupi
kula chakula cha pamoja na watoto wenye ualbino wanaolelewa kwenye kituo
cha Buhangija mjini Shinyanga kilichoandaliwa na Kampuni ya Ulinzi
Cyvalo Tanzania Limited inayomilikiwa na Crissant Mssipi.
Kabla
ya kula cha pamoja na watoto hao,mkuu huyo wa wilaya pamoja na
wafanyakazi wa kampuni hiyo ya ulinzi walifanya usafi wa mazingira
ikiwemo kupulizia dawa ya kuua wadudu kama vile kunguni katika mabweni
yanayotumiwa na watoto hao.
Hafla
fupi ya chakula cha pamoja iliyohudhuriwa pia na Afisa Mthibiti ubora
wa Shule halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Aziza Yanga,imenogeshwa
kwa burudani ya muziki ambapo Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Josephine
Matiro aliamua kucheza muziki na watoto hao hali iliyoongeza furaha
zaidi kwa watoto hao.Akizungumza katika kituo hicho,Matiro ameitaka
jamii kuondokana na dhana ya kuwabagua na kuwafanyia vitendo vya
kikatili ikiwemo kukata viungo na kuwaua akibainisha kuwa watoto wenye
ualbino binadamu kama wengine na kinacho watofautisha ni rangi tu ya
ngozi yao.
Amesema
jamii ikibadilika watoto hao wataishi kwa amani na furaha kwa kujiona
hawana tofauti na binadamu wengine ."Naomba jamii iondokane na matukio
ya kuwanyanyasa watoto hawa ili nao waishi kwa amani na upendo ,"
amesema Matiro.Aidha alisema hivi karibuni serikali iliamua kuwarudisha
majumbani baadhi ya watoto waliokuwa wanaishi katika kituo hicho
wakiwemo waliohitimu elimu yao ya msingi katika Shule ya Buhaghija hivyo
akaitaka jamii kuhakikisha inawalinda na wanaishi kwa amani bila ya
kubughudhiwa.
Naye
msemaji wa Kampuni hiyo ya Ulinzi Twaha Makani, amesema mara baada ya
siku chache kukitembelea kituo hicho waliguswa na vitu vingi vinavyohusu
maisha ya watoto hao na hivyo kuamua kufanya shughuli za usafi wa
mazingira, kupulizia dawa ya kuua kunguni pamoja na kula nao chakula cha
pamoja.
Kwa
upande wake mmoja wa walezi wa kituo hicho Bright Mduma mbali na
kuishukuru kampuni hiyo ya ulinzi kwa kufanya usafi,kuua wadudu na
kuandaa chakula,amesema kituo hicho kina jumla ya watoto 228, watoto
wenye ualbino 144, wasiosikia 60 na wasioona 24.Mwandishi wa Malunde1
blog,Marco Maduhu alikuwepo eneo la tukio ametuletea picha za matukio
yaliyojiri.
Mkuu
wa wilaya Josephine Matiro akizungumza katika hafla fupi ya kula
chakula cha pamoja na watoto wanaolelewa kituo cha Buhangija Mjini
Shinyanga ambapo aliwahakikishia ulinzi pamoja na kuboreshewa makazi
yao.-Picha zote na Marco Maduhu - Malunde1 blog
Msemaji
wa Kampuni ya Ulinzi Cyvalo Tanzania LTD inayomilikiwa na Crissant
Mssipi, bwana Twaha Makani akizungumza na watoto hao ambapo alisema
kampuni hiyo itaendelea kushirikiana nao kutatua baadhi ya changamoto
ambazo zinaendelea kuwakabili.
Msemaji
wa Kampuni ya Ulinzi Cyvalo Tanzania LTD inayomilikiwa na Crissant
Mssipi, bwana Twaha Makani akizungumza katika kituo cha Buhangija
Afisa
Mthibiti ubora wa shule halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Aziza
Yanga, akizungumza na watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija
ambapo aliwataka wadau wajitokeze kuwasaidia kutatua baadhi ya
changamoto zinazowakabili pamoja na kushiriki kula nao chakula cha
pamoja na siyo kusubiri hadi siku za sikukuu.

Wafanyakazi
wa Kampuni ya Ulinzi Cyvalo Tanzania LTD wakipulizia dawa ya kuua
kunguni katika mabweni ya watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija

Zoezi la kupulizia dawa ya kuua wadudu likiendelea

Sehemu ya Mashuka yakiwa yameanikwa baada ya kufuliwa na wafanyakazi wa kampuni hiyo
Mkuu wa wilaya Josephine Matiro akipika chakula kwa ajili ya watoto wenye ualbino katika kituo cha Buhangija mjini Shinyanga.
Watoto
wenye ualbino wakila chakula cha pamoja na mkuu wa wilaya ya Shinyanga
Josephine Matiro ,kilichoandaliwa na Kampuni ya Ulinzi Cyvalo Tanzania
LTD
Watoto
wanaolelewa katika kituo cha Buhangija wakila chakula cha pamoja na
mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro ,kilichoandaliwa na Kampuni
ya Ulinzi Cyvalo Tanzania LTD
Watoto wakiendelea kula chakula
Baadhi ya walinzi wa kampuni hiyo nao wakishiriki kula chakula cha pamoja na watoto hao
Zoezi la kula chakula likiendelea
Watoto wakila chakula
Mtoto akimuonesha mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro (aliyevaa nguo nyekundu) uwezo wake wa kucheza muziki
Mkuu
wa wilaya Josephine Matiro (aliyevaa nguo nyekundu) akicheza muziki
wimbo wa Diamond Platnumz zilipendwa na watoto wenye ualbino katika
kituo cha Buhangija
Mimi ni nomaaaa!! subiri nikuoneshe kazi mkuu.......
Mkuu wa wilaya Josephine Matiro akifurahia show ya mtoto.....
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akicheza na watoto hao
Kushoto ni Afisa Mthibiti ubora wa shule halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Aziza Yanga akicheza muziki
Watoto wakicheza mziki wa Kamatia chini
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akicheza Kwaito na watoto hao
Watoto wakicheza muziki na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro
Watoto wakisakata rhumba
Watoto wakiendelea kucheza
No comments:
Post a Comment