Kundi
la Tanzania One Theatre (TOT Plus), limo kambini Wanamuziki wake
wakijifua vikali katika mazoezi ya nyimbo tatu ambazo kundi hilo
litaziipua hivi karibuni.
Akizungumza
wakati wa mazoezi ya nyimbo hizo, Mkurugezi wa TOT Plus inayomilikiwa
na Chama Cha Mapinduzi (CCM), Gasper Tumaini amezitaja nyimbo hizo kuwa
ni 'Tumuunge mkono JPM', 'Amani ya Tanzania' na Hongera awamu ya tano'.
Tumaini
amsema, wimbo wa 'Tumuunge mkono JPM' ni wa kuwahamasisha Watanzania
popote walipo kumuunga mkono Rais Dk John Magufuli katika vita ya uchumi
anayoongoza kwa kuhakikisha inaziba mianya inayotishia upotevu au
matumizi mabaya ya rasilimali za nchi.
"Kama
unavyoona Rais tayari ameshaamua kwa dhati kupigana katika vita ya
kubana mianya inayotishia upotevu au matumizi mabaya yanayofanya na
baadhi ya watu kutumia rasilimali za nchi vibaya kwa kujinufaisha wao
huku taifa likiendelea kuwa masikini
Hii
siyo vita ndogo, ni kubwa sana inayohitaji ujasiri na ari kubwa ya
kujituma, hivyo ni lazima Watanzania wote tumuunge mkono ili
asiyumbishwe na waliokuwa wanajinufaisha na rasilimali hizi", alisema
Tumaini wakati wa mazoezi ya nyimbo hizo kwenye ukumbi wa Ofisi ya CCM
Mwinjuma, Mwananyamala, Dar es Salaam.
Amesema,
wimbo wa 'Amani ya Tanzania' kunahimiza Watanzania ndani na nje ya Nchi
kuhakikisha pia wanaienzi amani ya nchi kwa kuunga mkono juhudi za
kuiimanrisha zinazofanywa na viongozi wakiongozwa na misingi imara
iliyowekwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere na pia Rais wa Kwanza
wa Zanzibar Hayati Sheikh Abeid Amani Karume.
Akizungumzia
wimbo wa tatu wa 'Hongera awamu ya Tano', Tumaini amesema, wimbo huo ni
wa pongezi kwa Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli kwa kutimiza
kwa vitendo ahadi zilizotolewa na CCM wakati wa kampeni za kuomba ridhaa
ya wananchi katika uchaguzi mkuu uliopita.
"Tumeona
ni vizuri kutunga wimbo huu wa kumpongeza kwa sababu utekelezaji wa
ilani na ahadi alizokuwa akizitoa kwenye kampeni unaonekana wazi
japokuwa sasa ni miaka miwili tu tangu tumchague, kwa kweli Rais Dk.
Magufuli amechapa kazi hivyo inastahili kumpongeza", alisema tumaini.
Amesema,
nyimbo hizo ambazo ni kwaya tayari zimeshakamilika na sasa wanamuziki
wanazifanyia mazoezi ya mwisho mwisho kabla ya kuzirekodi ili zianze
kusikika katika maeneo mbalimbali na hasa pale kundi hilo litakapokuwa
likitumbuiza.
Mmiliki
wa theNkoromoBlog aliyefika kwenye mazoezi ya kundi hilo, alishuhudia
wanamuziki wote wakiwajibika kila mmoja katika eneo lake, huku baadhi
yao wakitokwa jasho kuliko hata wanapokuwa wakitumbuiza jukwaani katika
maonyesho maalum.
Mwanamuziki
nguli Juma Abdallah 'Jerry' akikipapasa kinanda kwa mkoni mmoja
kuonyesha umahiri wake, Kundi la TOT Plus lilipokuwa katika mazoezi ya
nyimbo tatu, leo katika ukumbi wa CCM Mwinjuma, Mwananyamala Dar es
Salaam
Waimbaji
Neca Twalib aliyechukua nafasi iliyoachwa na aliyekuwa mwimbaji nguli
na Mkurugenzi wa TOT Plus Marehemu Kampteni John Komba, akiimba na
mwenzake Corobian Mkinga wakati wa mazoezi hayo
Patrick Thomas akizicharaza tumba wakati wa mazoezi hayo
Mkurugenzi wa TOT Plus Gasper Tumaini (mwenye suti) akizungumza na baadhi ya wadau waliofika kushuhudia mazoezi hayo
Jerry akikicharaza kinanda kwa madaha wakati wa mazoezi hayo
Waimbaji Rosemary William, Sharifa Mohammed na Mwasiti Suleimani wakiimba wakati wa mazoezi hayo
Mwimbaji nguli Hadija Kopa na wenzake wakiimba wakati wa mazoezi hayo
Tumaini akiwa na wadau wakati wakifuatilia mazoezi hayo. Kulia ni Jerry
Waimbaji wa TOT Plus wakiwa kwenye mazoezi hayo
Waimbaji wa TOT Plus wakiwa kwenye mazoezi ya wimbo wa 'Amani ya Tanzania'
Jerry na Tumaini wakifuatilia kwa makini mazoezi hayo. Kushoto ni mdau wa TOT Plus
Alen Elias aka Mchungaji akikicharaza kinanda kwa makini
Evans Peter na said Mpiluka wakiyacharaza magita wakati wa mazoezi hayo
Godfrey Kanuti akilicharaza gita wakati wa mazoezi hayo
Neka twalib na Mkinga wakishauriana jambo wakati wa mazoezi hayo
Fundi mitambo akiwajibika wakati wa mazoezi hayo
Tumaini akijadiliana jambo na viongozi wa bendi ya Vijana Jazz ambao walihudhuria mazoezi hayo
Wanamuziki wa TOT Plus wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wadau wakati wa mazoezi hayo
No comments:
Post a Comment