Baadhi
ya vikundi vya wajasiriamali wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa
Wilaya ya Kisarawe wakati wa sherehe za kukabidhiwa hundi ya kiasi cha
shilingi milioni 102 kwa ajili ya mikopo ambayo iatawasaidia katika
kuendeshea shughuli zao za biashara pamoja na ujenzi wa viwanda vidogo
vidogo.
Mkuu
wa Wilaya Kisarawe Happiness Seneda aliyesimama akizungumza na vikundi
vya wajasiriamali kutoka kata mbali mbali katika halfa fupi ya
kukabidhiwa hundi ya kiasi cha shilingi milioni 102 kwa ajili mkopo wa
kuwawezesha kiuchimi.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Happiness Seneda akizungumza jambo katika halfa fupi ya vikundi vya wajasiriamali.
Mkurugenzi
mtendaji wa halmashari ya Kisarawe Mussa Gama akizungumza na vikundi
vya wajasiriamari hao hawapo pichani kabla ya kukabidhiwa hundi hiyo ya
kiasi cha shilingi milioni 102 kwa ajili ya kuwawezesha mikopo kwa ajili
ya kujikwamua kiuchumi.
PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGU
……………..
NA VICTOR MASANGU, KISARAWE
HALMASHAURI
YA wilaya ya Kisarawe iliyopo Mkoani Pwani katika kuunga mkono juhudi
za Rais wa awamu ya tano Dk. John Pombe Magufuli kuwa na uchumi wa
viwanda imetoa kiasi cha shilingi milioni 102 kwa vikundi vya
wajasiriamali vipatavyo 49 vya wakinamama,vijana pamoja na walemavu kwa
lengo la kuweza kuwasaidia kuendesha shughuli zao mbali mbali za
biashara mbali mbali ikiwemo na kuwawezeha ili waweze kujikita zaidi
katika kujenga viwanda vidogo vidogo.
Akizungumza
katika halfa fupi ya kukabidhi hundi ya fedha hizo iliyohuduriwa na
viongozi mbali mbali wa serikali pamoja na viongozi wa vikundi hivyo
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Mussa Gama
alisema kwamba fedha hizo za mikopo zimetolewa kwa vikundi hivyo kutokea
kata zote 17 ambapo zimetokana na makusanyo ya mapato ya ndani.
Mkurugenzi
huyo alibainisha kuwa kutaweza kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo
na kuweza kukuza uchumi wa nchi kutokana na kuweza kuwapa fursa
wajarisiamali hao kupania wigo wa kibiashara pamoja na kuanzissha
viwanda vingine vidogo vidogo ambayo vitaweza kuongeza upatikanaji wa
ajira mpya na kupunguza wimbi la umasikini.
“Kwa
kweli sisi kama halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe tumejipanga kuweka
mipango madhubuti katika kuviwezesha vikundi vyetu vya ujasiriamali kwa
kutumia fedha zetu ambazo zinatokana na makusanyo ya mapato ya nadani,
hivyo vikundi hiivi ni moja ya mipango yetu katika kuhakikisha ile
asilimia 10 iliyotengwa inawafikia walengwa na kuweza kuleta mabadiliko
chanya ya kimaendeleo,”alisema Mkurugenzi huyo.
Kwa
upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Happiness Seneda ameviasa vikundi
vyote vilivyopata mkopo huo hususan kwa wakinamama kuachana kabisa na
vitendo vya kutumia fedha hizo vibaya kwa shughuli ambazo hazina manufaa
yoyote kwa jamii, kama vile kuwachezesha watoto wao ngoma wakati wa
kufunga shule pamoja na kununulia madela kitu ambacho amekilaani vikali.
Aidha
Seneda alisema kuwa malengo ya serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha
wananchi wake wanawezeshwa kwa namna mbali mbali ikiwemo kuwapatia
mikopo ambayo itaweza kuwapa fursa ya kukuza biashara zao pamoja na
wengine kufanya biashara zao ndondogo amabzo zitaweza kuwapatia kipato
na kujikwamua kiuchumi.
“Jamani
mimi kama kiongozi wenu napenda kuwaasa wale wote mlionufaika na mkopo
huu, kuhakikisha mnazitumia vizuri fedha hizi hasa kwa upande wa
wakinamama ambao wamekuwa na tabia pindi wanapotata pesa wanazitumia
katika matumizi mengine ya kununulia madela kwa ajili ya sare pamoja
shughuli nyingine kama vile kuwacheza ngoma watoto wao hii tabia kwa
kweli sipendi kuiona katika Wilaya yangu,”alisema Seneda.
Nao
baadhi ya wajasiriamali ambao wamenufaika na mkopo wa fedha hizo akiwemo
Monica Muhoza ambaye ni mlemavu wa miguu, Faudhia Kasikasi, pamoja na
Gudluck Akyoo wameshukuru uongozi mzima wa halmashauri ya Kisarawe na
kusema kuwa fedha hizo walizopatiwa ni mkombozi mkubwa kwa upande wao
kwani zitaweza kuwasaidia kujikwamua kiuchumi pamoja na kujikimu
kimaisha na kuendesha familia zao.
VIKUNDI
hivyo vya wajasiriamali 49 kutoka kata 17 za Wilayani Kisarawe
zimewahusiha wakinamama, vijana, pamoja na makundi vya walemavu ambapo
vimepata mkopo wa fedha hizo kiasi cha shilingi milioni 102 ikiwa ni
makusanyo ya mapato ya fedha za ndani.
No comments:
Post a Comment