A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Monday, October 2, 2017

Waliokula mil 359/- za barabara zawakwama

Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Barabara (RFB), Joseph Haule
BODI ya Mfuko wa Barabara imeziamuru halmashauri saba nchini zilizotumia zaidi ya Sh milioni 359.5 zilizotolewa kwa ajili ya kujengea barabara, lakini zikazitumia kununua madawati na kujengea maabara kuzirudisha mara moja katika mfuko huo.
Halmashauri hizo ni Karagwe Sh milioni 55.5, Kyerwa Sh milioni 36.8, Ushetu Sh milioni 15.7, Masasi Mji Sh milioni 31.3, Nanyumbu Sh milioni 110.7, Kilolo Sh milioni 102.3 na Songea ya Mji Sh milioni 7.3, na zinatakiwa kurudishwa fedha hizo kabla ya Oktoba 30, mwaka huu. Hayo yalisemwa mjini Dodoma jana na Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Barabara (RFB), Joseph Haule wakati akiwasilisha taarifa ya ukaguzi wa kiufundi na fedha kwa kazi za ujenzi na matengenezo ya barabara na madaraja kwa mwaka wa fedha 2014/15 na 2015/16.
“Kwa zile halmashauri za wilaya zilizotumia fedha za Mfuko wa Barabara kwa matumizi mengine kama vile kutengenezea madawati na ujenzi wa maabara, wakaguzi wa halmashauri husika wahakikishe zinarudisha haraka katika akaunti ya Mfuko wa Barabara ya Dharura,” alisema Haule na kufafanua kuwa halmashauri hizo zilikiuka Sheria ya Fedha ya Mwaka 2001, Sheria ya Manunuzi ya Umma ya mwaka 2011 na Sheria ya Tozo za Barabara na Mafuta na Kanuni zake.
Pia kuna halmashauri ambazo zililipia jumla ya Sh milioni 87.1 kwenye kazi hewa ambazo hazijafanyika ambazo ni pamoja na Mtwara ambayo ililipa Sh milioni 46.2, Tanga Mjini Sh milioni 12.1, Monduli Sh milioni 6.6, na Moshi Sh milioni 12.2 nazo zinatakiwa kulipa fedha hizo. Halmashauri ya Gairo ambayo miradi mingi haijatekelezwa kadiri ya mikataba ya makubaliano, ilipewa nafasi ya kufika mbele ya Bodi ya Mfuko, lakini ilichelewa kufika.
“Halmashauri ya Kalambo, mkandarasi wake aliidhinisha malipo ya Sh milioni 15.4 ya kupima kifusi ambacho hakijashindiliwa kinyume cha mkataba unaotaka kuidhinisha malipo kifusi kilichoshindiliwa,” alisema na kubainisha kuwa Halmashauri ya Kakonko ilihamisha Sh milioni 13.7 zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya mradi wa matengenezo ya barabara na kutekelezea mradi mwingine, kinyume cha mkataba wa makubaliano. "Halmashauri ya Kondoa ilipewa zaidi ya Sh milioni 60 kwa ajili ya kujenga maeneo korofi na ikajenga chini ya kiwango na hivyo kuisababishia hasara kubwa serikali," alisema.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages