A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Monday, October 2, 2017

Filamu zaidi ya 150 kushindanishwa Tamasha la kitaifa la Sinema zetu

Kituo cha Azam Tv leo kimetangaza Tamasha jipya la Kimataifa litakaloitwa Tamasha la kitaifa la Sinema zetu kwa lengo la kupanua wigo wa tasnia ya filamu za kiswahili nchini kwa kuwezesha watu kuona filamu za kiswahili zenye maudhui ya utamaduni wetu.
Akizungumza na waandishi wa habari Mratibu wa Tamasha hilo Zamaradi Nzowa amesema kuwa tamasha hilo litasaidia kukuza taaluma ya filamu na kuongeza ubunifu na kutambua ubora wa ufanisi katika tasnia ya filamu.

Amesema kuwa tamasha hilo pia litaonyesha filamu zaidi ya 150 na kutoa tuzo kwa washiriki mbalimbali katika taaluma tofauti za tasnia hiyo.

Naye Mkurugenzi wa tamasha hilo Jacob Joseph amesema kuwa kupitia tamasha hilo wamebuni mbinu maalum ili kuwafikia wadau wa tasnia duniani kote.

Amesema ili kuhakikisha kuwa wanawafikia wadau wote Afrika mashariki watakuwa na vituo maalum mikoani na katika nchi za Afrika mashariki ili kueneza, kuhamasisha na kupokea filamu zitakazowasilishwa katika mashindano.
Amesema vituo hivyo vitakuwa katika Mikoa ya Morogoro, Zanzibar, Tanga, Arusha, Mwanza, Mbeya, Dodoma na Mtwara lakini pia Nairobi, Kampala, Kigali, Bujumbura na Goma.

Kwa upande wake balozi wa tamasha hilo Elizabeth Michael maarufu kama Lulu amesema kuwa uzuri wa tamasha hilo ni kuwa filamu zote zinaweza kushindanishwa na hakuna upendeleo wowote.

Amesema jopo la waamuzi ni la kimataifa na litahakikisha haki inatendeka na uwepo wa jopo hilo la watu 25 linatokana na wadau tofauti wa tasnia.

Hata hivyo katika tamasha hilo kutatolewa tuzo ambazo zitakuwa na fedha itakayofikia milioni 5 kwa filamu bora na filamu zitakazo shindanishwa ni Bongo movie, filamu fupi na filamu za makala.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages