Wajumbe
wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Wauguzi Tanzania (TANNA) kutoka sehemu
mbalimbali wakiungana na wajumbe wenzao pamoja na viongozi wa Tanna Mkoa
wa Lindi jana katika kufanya maandalizi ya Mkutano Mkutano Mkuu wa 45
unao tarajiwa kufanyika Oktoba 4-6 Kitaifa ambapo Mgeni rasmi
anatarajiwa kuwa Mh. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Kassim Majaliwa.( PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)
Mwenyekiti
wa Chama Cha Wauguzi Tanzania (TANNA) Mkoa wa Lindi, Patrick Achimpota
(kulia) mwenyeshati la kitenge akisalimiana na mjumbe wa Kamati kuu ya
Chama hicho kutoka Arusha, Hosea Naman mara alipofika Mkoani humo kwa
niaba ya Mkutano Mkuu wa Chama hicho.
Wajumbe
wa Chama Cha Wauguzi (TANNA) wakiwa katika safari kuelekea Mkoa wa
Lindi katika Mkutano Mkuu wa Chama hicho unao tarajiwa kufanyika Oktoba
4-6 Kitaifa ambapo unatarajiwa kufunguliwa na Waziri Mkuu, Kasim
Majaliwa.
Muuguzi
Mkuu wa Hospitali ya Mkoa Lindi, Damasiana Msala (kulia) akizungumza
na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Wauguzi (TANNA) mara
walipowasili katika mkoa huo jana
Makamu
wa Rais wa Chama hicho, Ibrahim Mgoo (wa katikati) akisalimia wajumbe
mara baada ya kuwasili katika Mkoa huo jana, kulia ni Muuguzi Mkuu wa
Hospitali ya Mkoa Lindi, Damasiana Msala na kushoto ni Katibu Mkuu wa
Chama hicho, Sebastian Luziga
Katibu Mkuu wa Chama hicho, Sebastian Luziga (kushoto) akisalimia wajumbe mara walipowasili jana Mkoani Lindi, kulia ni Muuguzi Mkuu wa Hospitali ya Mkoa Lindi, Damasiana Msala na Makamu wa Rais wa Chama hicho, Ibrahim Mgoo
Mkurugenzi
wa Maendeleo wa Chama cha Wauguzi (TANNA), Charles Soloka (kushoto)
atowa taarifa ya majumuoisho ya maandalizi ya Mkutano huo jana
No comments:
Post a Comment