Wadau wa masuala ya sekta ya aAdhi wakiwa katika picha ya pamoja.Kaimu
Mkurugenzi wa TEHAMA kutoka Wizara ya Ardhi akitoa ufanunuzi juu ya
ujenzi wa Mfumo unganishi wa taarifa za sekta ya Ardhi (ILMIS).Wadau
wa Sekta ya Ardhi wakisiliza taarifa kuhusu mfumo unganishi wa taarifa
za
Wizara
ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeendesha warsha ya kuwajengea
uwezo wadau wa masuala ya sekta ya ardhi nchini kuhusu mifumo
mbalilmbali inavyotumika katika kutoa huduma kwa wananchi.
Akifungua
warsha hiyo Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Dkt. Moses Kusiluka
alisema, hadi sasa wizara inatumia mfumo zaidi ya mmoja kutoa huduma za
kila siku kwa mwananchi. Uwepo wa mifumo hiyo katika utoaji huduma za
sekta ya ardhi ni muhimu kwa ajili ya kurahisisha huduma. Ili kufikia
malengo, ni lazima kuwepo na mfumo mmoja utakaounganisha mifumo yote
hiyo kwa lengo la kuongeza ufanishi na kuboresha huduma.
Uundaji wa mfumo unganishi wa taarifa za sekta ya ardhi (Intergrated Land Management Information System, ILMIS)unatekelezwa
na Wizara ya Ardhi, nyumba na Maendeleo ya Makazi ikishiriana na
wataalamu kutoka kampuni ya IGN FI kwa udhamini wa Benki ya Dunia.
Uundaji huu ulishaanza na kwa sasa mfumo uko katika hatua ya majaribio.
Dhumuni
kuu la uundaji mfumo unganishi wa taarifa za sekta ya ardhi ni
kuimarisha usalama katika umiliki wa ardhi kwa kuboresha usahihi katika
taarifa za ununuzi ardhi, usajili, upimaji na pia katika kusimamia ardhi
kwa ujumla wake.
Utekelezaji
wa Mfumo unganishi wa taarifa za sekta ya ardhi (ILMIS), utahusisha
mambo mbalimbali kama vile njia rahisi na rafiki ya kusimamia uundaji na
uendelezaji wa mfumo wenyewe, majaribio ya mfumo katika utekelezaji,
ubadilishaji wa taarifa za ardhi zilizopo mfano taarifa za upimaji na
ramani, hatimilki na kuziweka katika mfumo.
Naye
Msajili Msaidizi wa Hati, Appolo Laizer alisisitizia umuhimu wa
utumiaji mfumo unganishi wa taarifa za sekta ya ardhi (ILMIS) kwa wadau
wa sekta ya ardhi alipokuwa akielezea jinsi hatimilki zitakavyotolewa na
mfumo huo.
Alisema,
utoaji wa hati kupitia mfumo utaongeza usalama katika nyaraka za
umiliki, huduma sahihi, salama na kwa unafuu zaidi. Mfumo utapunguza
muda wa kuhakiki taarifa katika uhamisho wa milki kutoka kwa mtu mmoja
kwenda kwa mwingine, kuongeza ulinzi kwenye maeneo yaliyotengwa kama
hifadhi ya barabara, misitu au maeneo ya wazi.
Utoaji
wa hatimilki kwa kutumia mfumo utasaidia sana kupunguza kama sio
kumaliza kabisa migogoro ya ardhi kwa kulinda umiliki wa mwananchi. Pia
mfumo utaondoa migogoro ya umilikishaji wa hati kwa mtu zaidi ya mmoja
pamoja na kuongeza ulinzi wa hatimilki katika taasisi za kifedha.
No comments:
Post a Comment