A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Monday, October 2, 2017

MKUTANO WA JUMUIYA YA SERIKALI ZA MITAA TANZANIA (ALAT) WA ANZA RASMI

Image result for PICHA MEYA WA JIJI

Mkutano wa 33  Jumuiya  ya Serikali za mitaa Tanzania ( ALAT)  leo umeanza rasmi jijini Dar es salaam  , ambapo Meya wa jiji la Dar es salaam isaya Mwita amewapokea wajumbe wa mkutano huo kutoka sehem mbalimbali  za mikoa ya Tanzania.

Akizungumza katika  ukaribisho huo Meya Isaya  amesema mkutano huo unatarajiwa  kufunguliwa rasmi kesho na rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania mhe. Dr John Pombe Magufuli ambapo wajumbe hao wataendelea vikao hadi tarehe 6 octoba  kujandili mambo mbali mbali yanayo zikabili serikali za mitaa.

Aidha amesema jumuia hiyoinatarajiwa kuwasilisha maombi rasmi kwa Rais Magufuli ili vyanzo vya mapato vilivyo chukuliwa na serikali kuu viweze kurudishwa katika  Halmashauri iliziweze kuongeza uwezo wa kujiendesha .
 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje Mkoani Songwe , Haji Mnasi ,ameiambia  kilole mzee blog kuwa kupitia mkutano huo wanatarajia kujifunza  namna  ya kukabiliana na changamoto  najinsi  ya kuleta maendeleo katika  halmashauri zao na kubadilishana uzoefu kitu ambacho kitasaidia kuweza kuwasaidia wananchi kupata huduma bora za kijamii na kufikia adhima ya Rais ya Tanzania ya  viwanda .

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages