Mkurugenzi
Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa akizungumza
wakati wa kufunga mafunzo ya wadadisi wa Utafiti wa Takwimu za Kilimo
kwa mwaka 2016/17 mkoani Dodoma. Utafiti huo wa Takwimu za Kilimo
utafanyika nchi nzima kuanzia tarehe 3 Oktoba na kumalizika tarehe 3
Novemba, 2017.
Mgeni
rasmi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Maria
Mashingo akihutubia wakati wa kufunga mafunzo ya wadadisi wa Utafiti wa
Takwimu za Kilimo kwa mwaka 2016/17 mkoani Dodoma. Utafiti huo wa
Takwimu za Kilimo utafanyika nchi nzima kuanzia tarehe 3 Oktoba na
kumalizika tarehe 3 Novemba, 2017.
Baadhi
ya wadadisi wa Utafiti wa Takwimu za Kilimo kwa mwaka 2016/17
wakifuatilia kwa makini hotuba ya mgeni rasmi (hayupo pichani) wakati wa
kufunga mafunzo ya utafiti huo mkoani Dodoma. Utafiti huo wa Takwimu za
Kilimo utafanyika nchi nzima kuanzia tarehe 3 Oktoba na kumalizika
tarehe 3 Novemba, 2017.
Mgeni
rasmi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Maria
Mashingo (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa NBS,
Chuo cha Mipango na baadhi ya wadadisi wa Utafiti wa Takwimu za Kilimo
kwa mwaka 2016/17. Utafiti huo wa Takwimu za Kilimo utafanyika nchi
nzima kuanzia tarehe 3 Oktoba na kumalizika tarehe 3 Novemba, 2017.
Mwanasheria wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Oscar Mangula akiwaapisha wadadisi wa Utafiti wa Takwimu za Kilimo kwa mwaka 2016/17 baada ya kufunga mafunzo ya utafiti huo mkoani Dodoma. Utafiti huo wa Takwimu za Kilimo utafanyika nchi nzima kuanzia tarehe 3 Oktoba na kumalizika tarehe 3 Novemba, 2017.
Na: Veronica Kazimoto
Serikali
kupitia Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) inatarajia kufanya Utafiti wa
Kilimo wa mwaka 2016/17 nchi nzima kuanzia kesho tarehe 3 Oktoba hadi
tarehe 3 Novemba, 2017.
Akizungumza
leo wakati wa kufunga mafunzo ya wadadisi watakaokusanya Takwimu za
Kilimo kwa mwaka 2016/17 mkoani Dodoma, Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo,
Mifugo na Uvuvi Dkt. Maria Mashingo amesema lengo la utafiti huo ni
kutoa makadirio ya kiasi cha uzalishaji wa mazao makuu, idadi ya mifugo,
mazao yatokanayo na mifugo na maeneo ya kilimo katika mikoa yote ya
Tanzania.
"Ningependa
kuwasisitizia washiriki kuwa, dhumuni kubwa la utafiti huu wa kilimo
ni kutoa makadirio ya uzalishaji wa mazao makuu ya kilimo na maeneo yake
yaliyolimwa pamoja na taarifa za mifugo katika mikoa yote ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania", amesema Dkt. Mashingo.
Aidha,
Katibu Mkuu huyo ametoa wito kwa wakuu wote wa kaya watakaochaguliwa
kushiriki kwenye utafiti huu, kutoa ushirikiano wa kutosha na hususan
kutoa taarifa sahihi kuhusu hali ya uzalishaji wa mazao, huduma
zinazotolewa na Maafisa Ugani na aina ya mbegu wanazotumia na kubainisha
changamoto wanazokumbana nazo katika shughuli zao za kila siku.
Nae
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa amesema
jumla ya wadadisi 600 wamepatiwa mafunzo ya siku 5 kwa ajili ya kufanya
utafiti huo nchi nzima.
Dkt.
Chuwa amefafanua kuwa madhumuni ya mafunzo kwa wadadisi hao ni
kuwajengea uwezo wa kuhoji na kujaza madodoso ya wamiliki wa mashamba
(wakulima) na namna ya kutambua mahali shamba lilipo kwa kutumia kifaa
maalumu kiitwacho GPS.
Utafiti
huu wa Kilimo wa mwaka 2016/17 unafanyika chini ya Ofisi ya Taifa ya
Takwimu (NBS) na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu, Zanzibar (OCGS) kwa
kushirikiana na Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na Wizara ya Viwanda,
Biashara na Uwekezaji.
No comments:
Post a Comment