Majaji
wa Mahakama Kuu ya Zanzibar wakipitia hati zao za viapo kabla ya
kuapishwa Rasmi na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) kushika wadhifa walioteuliwa
hafla ya kiapo ilifanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar.
Baadhi
ya Majaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar ni miongoni mwa Viongozi mbali
mbali waliohudhuria katika hafla ya kiapo cha Majaji wa Mahakama Kuu ya
Zanzibar walioapishwa leo na Viongozi wengine kazi iliyofanya na Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
(hayupo pichani) Ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar.
Viongozi
waliohudhuria katika hafla ya kuapishwa Majaji wa Mahakama Kuu ya
Zanzibar katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar leo, (kutoka kulia)
Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi, Kadhi Mkuu wa Zanzibar
Sheikh Khamis Haji na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Katiba,
Sheria,Utumishi wa Umma na Utawala Bora Khamis Juma Maalim.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
(kushoto) akimuapisha Bw. Khamis Ramadhan Abdala kuwa Jaji wa Mahakama
Kuu ya Zanzibar katika hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu
Mjini Zanzibar.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
(kushoto) akimuapisha Bibi Aziza Iddi Suwedi kuwa Jaji wa Mahakama Kuu
ya Zanzibar katika hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini
Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed
Shein (kushoto) akimuapisha Bw. Kubingwa Mashaka Simba kuwa Katibu wa
Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma katika hafla iliyofanyika leo
katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,kabla alikuwa Naibu Katibu Mkuu
Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
(kushoto) akimuapisha Bw. George Joseph Kazi kuwa Naibu Katibu Mkuu
Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora katika
hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar, kabla
alikuwa Mrajis wa Mahakama Kuu ya Zanzibar.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi na Majaji wa
Mahakama Kuu ya Zanzibar, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Katiba,
Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora na Katibu wa Tume ya Maadili ya
Viongozi wa Umma baada ya kuwaapisha rasmi leo katika hafla
iliyofanyika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar (Picha na Ikulu).
No comments:
Post a Comment