Meneja
Ufuatiliaji na Tathimini mradi wa Data kwa Maendeleo ya Jamii wa Tume
ya Sayansi na Teknolojia, Dk. Geofrey Chambua akiongea mbele ya
wanahabari jijini Dar es Salaam wakati wakimtambulisha mfumo mpya wa
kieletroniki wa ‘Dopwall’. Pembeni ni Mkurugenzi Mkuu Kampuni ya Eagle
Analytics, Rose Funja ambao ni wasimamizi wa mfumo huo.
Mkurugenzi
Mkuu Kampuni ya Eagle Analytics, Rose Funja ambao ni wasimamizi wa
mfumo huo akifafanua machache mbele ya wanahabari jijini Dar es Salaam
jinsi mfumo huo unavyofanyakazi. Pembeni ni Meneja Ufuatiliaji na
Tathimini mradi wa Data kwa Maendeleo ya Jamii wa Tume ya Sayansi na
Teknolojia, Dk. Geofrey Chambua.
MFUMO
mpya wa kieletroniki wa ‘Dopwall’ umezinduliwa nchini na unatajwa kuwa
utasaidia kupunguza mdondoko wa elimu kwa wananchi wa kike nchini.
Licha
ya hali hiyo pia inatajwa kuwa mdondoko wa wanafunzi kwa shule bado ni
tatizo nchini ambapo kwa kipindi cha mwaka 2015 wanafunzi 61,488
waliripotiwa kuacha masomo.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam juzi Mkurugenzi Mkuu Kampuni ya Eagle Analytics,
Rose Funja, alisema kuzinduliwa kwa mfumo huo kusaidia wazazi na walezi
kujua hali ya maendeleo ya shule wanasoma watoto wao ikiwemo kuwa na
uwezo wa kuhoji kupitia vikao vya wazazi na bodi za shule.
“Serikali
kupitia wizara mbalimbali ikiwemo Serikali za Mitaa wameboresha
ukusanyaji wa taarifa mbalimbali za kielimu ambazo ni msingi wa
mapambano dhidi ya mdondoko wa wanafunzi. Pamoja na jitihada hizo
matumizi ya taarifa kama hizo katika kuboresha utendaji wa kila siku wa
watumishi wa umma na ufanyaji wa maamuzi hayatoshelezi au hakuna kabisa
katika idara za serikali,” alisema Funja
Kwa
upande wake Meneja Ufuatiliaji na Tathimini mradi wa Data kwa Maendeleo
ya Jamii wa Tume ya Sayansi na Teknolojia, Dk. Geofrey Chambua, alisema
mfumo wa kieletroniki wa ‘Dropwall’ unalenga kuongeza matumizi ya
taarifa zinazokusanywa na wadau mbalimbali ikiwemo serikali.
“Ubunifu
wa mfumo huu umedhaminiwa na mradi wa Data fot Local Impact (DLI) ikiwa
ni moja kati ya miradi mitatu ya takwimu inayosimamiwa na MCC pamoja na
PEPFAR. Udhamini wa dli uliwesha uchunguzi wa mdondoko mashuleni katika
wilaya za Mbeya na Nzega chini ya mwongozo wa TAMISEMI.
“Kampuni
ya Eagle Analytics inayotengeneza mfumo wa Dropwall ni kampuni changa.
Mhandisi Rose na timu yake kupitia ubunifu wao wa kubaini uwezekano wa
mwanafunzi kuacha masomoni mmoja wa washindi 12 wa shindano la ubunifu
lililoratibiwa na DLI ikishirikiana na Tume ya Sayansi na Teknolojia
(COSTECH) mwaka 2016,” alisema Dk. Chambua.
No comments:
Post a Comment