A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Sunday, September 24, 2017

WADAU WAZIDI KUJITOKEZA KUMUUNGA MKONO RC MAKONDA UJENZI WA OFISI ZA WALIMU

Kamati ya Ujenzi wa Ofisi 402 za Walimu kwa Mkoa wa Dar es Salaam imepokea msaada wa matofali 1000 kutoka kwa kampuni ya A and Bel Impex Tanzania Limited kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za walimu wilaya ya Kigamboni.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Afisa Elimu Mkoa wa Dar es Salaam Hamis Lissu amesema wanaipongeza kampuni hiyo kwa kujitolea msaada huo huku akieleza kuwa utasaidia katika kuboresha elimu kwa ujenzi wa ofisi za walimu kwani katika shule 513 za Mkoa wa Dar es Salaam asilimia kubwa ya takribani shule zaidi ya 400 hazina ofisi za walimu jambo ambalo ni changamoto katika maendeleo ya elimu.

Lissu amesema  kuwa ujenzi wa ofisi 402 za walimu kwa Mkoa wa Dar es Salaam utakamilika kwa muda wa miaka miwili ila utakuwa na awamu katika shule za kila wilaya ambapo ameelekeza matofali hayo 1000 yapelekwe shule ya Nguva Sekondari ya Wilaya hiyo ya Kigamboni na ujenzi uanze mara moja kuanzia hivi sasa.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa kampuni ya A and Bel Impex Tanzania Limited iliyotoa msaada wa matofali hayo bwana Thobias Hima ameeleza kuwa wameamua kuunga mkono jitihada za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda katika ujenzi wa ofisi za walimu na watahakikisha pale panapohitajika msaada wanafanya hivyo kwa maendeleo ya watanzania wote.

"Licha ya kutoa matofali haya 1000 tumetoa pia na mashine ya kufyatulia matofali na eneo la kufanyia shughuli hiyo la Mwembe Mdogo, Mtaa wa Minondo Kata ya Somangila" Alisema. 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa  Ofisi 402 za Walimu Kanali Charles Mbuge ameeleza kuwa ufyatuaji wa matofali utakuwa unafanyika majira ya usiku katika eneo hila la kata ya Somangila, huku akihimiza wadau mbalimbali kuwaunga mkono katika kufikia lengo la ujenzi wa ofisi hizo.


Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni David Mgonja ameeleza kuwa shule zitakazo pitiwa na mpango huo ni 12 na zitakuwa kwa awamu huku 4 zikiwa za sekondari na 8 za msingi, ambapo awamu ya kwanza itajumuisha shule mbili za sekondari na tatu za msingi, za sekondari zikiwa Nguva na Tungi, huku za msingi ni Mwongozo, Mizimbini na Vumilia Ukooni.


Afisa Elimu Mkoa wa Dar es Salaam Hamis Lissu akizungumza na waandishi wa habari alipokwenda kupokea matofali hayo.

Mwenyekiti wa kamati ya ujenzi wa ofisi 402 za walimu Mkoa wa Dar es Salaam, Kanali Charles Mbuge, akizungumza na baadhi ya wajumbe wa kamati ya ujenzi huo katika hafla hiyo.
Mkurugenzi wa kampuni ya A and Bel Impex Tanzania Limited ,Thobias Hima wa pili (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari mara baada yakukabidhi matofali hayo. wengine ni wanakamati wa ujenzi wa ofisi za walimu.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages